CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesisitiza kwamba maandamano ya amani ambayo yalipangwa kufanyika kesho nchi nzima yatafanyika.
Akizungumza na kulunzifikra blog, Edward Simbeye, katibu mwenezi wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha), amesisitiza kuwa maandalizi kwa ajili ya maandamano hayo yanaendelea vizuri na tayari chama hicho kilishaandika barua kulitaarifu jeshi la polisi kuhusiana na uwepo wa maandamano hayo katika kila mkoa nchini.
Aidha, kiongozi huyo amesema kuwa mpaka muda huu bado jeshi hilo halijajibu barua ambayo chama hicho kimeliandikia na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litakuwa halijajibu barua yao mpaka kufikia siku ya kesho.
“Maandalizi yanaendelea vizuri na hapo kesho tutatoa muongozo kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla kuhusiana na mahali ambapo maandamano hayo yataanzia na kuishia katika kila mkoa nchini.” amesema Simbeye
Akifafanua kuhusiana na tabia ya jeshi la polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano kwa sababu mbalimbali, Simbeye amesema kuwa maandamano ni haki ya kikatiba na jeshi la polisi lina wajibu wa kulinda wananchi ambao wanatumia haki yao ya kikatiba kufanya maandamano na si kuzuia maandamano na kuongeza kuwa maandamano hayo yatafanyika hata kama jeshi hilo litazuia maandamano hayo.
Wiki iliyopita, baraza hilo la vijana lilitangaza kuwepo kwa maandamano ya amani siku ya kesho ambayo waliyapa jina la “Black Thursday” yenye lengo la kushinikiza kuwepo kwa haki za kisiasa, kiuchumi, utawala wa sheria pamoja na haki za binadamu nchini.
Wednesday, 30 August 2017
Home
Unlabelled
Chadema yasisitiza kufanya maandmano ya amani kesho nchi mzima.
Chadema yasisitiza kufanya maandmano ya amani kesho nchi mzima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Vat leaching gold processing method is the recently technology that practised in developing nations. In Tanzania vat leaching method w...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
No comments:
Post a Comment