Sirro: Kibiti hali ni shwari - KULUNZI FIKRA

Saturday 26 August 2017

Sirro: Kibiti hali ni shwari

 
 Jeshi la polisi nchini limesema kuwa limefanikiwa kudhibiti uhalifu ulioukuwa unafanyika wilayani ya Kibiti mkoani Pwani na kuwakamata wahalifu wenyewe hatua ambayo imewezesha kurudisha hali ya usalama katika maeneo hayo.

Akiwa ziarani mkoani Arusha Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, amesema oparesheni hiyo imefanikiwa kuwakamata wengi wa waliokuwa wakifanya uhalifu ama kujihusisha nao na kutoa angalizo kwa viongozi ngazi za vijiji na kata katika maeneo yote nchini kuhakikisha wanakuwa makini kwani baadhi yao wamekimbilia katika maeneo mengine.

Aidha Kamshna Sirro ameeleza kuwa sehemu ya mazungumzo yake na askari polisi mkoa wa Arusha na kusema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kufanyia kazi malalamiko ya wananchi ikiwemo uvujaji wa siri za watoa taarifa na kuahidi kulivalia njuga suala hilo.

IGP Simon Sirro yupo katika ziara yake ya kikazi kutembelea na kuzungumza na askari polisi katika mkoa mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment

Popular