Sakata la IMMA:Rais wa TLS Tundu Lissu atoa maazimio ya baraza la uongozi - KULUNZI FIKRA

Sunday 27 August 2017

Sakata la IMMA:Rais wa TLS Tundu Lissu atoa maazimio ya baraza la uongozi

Mwanasheria  Tundu Lissu na  Rais wa chama cha mawakili Tanzania(TLS) wameongea nawaandishi wa habari na ameanza kwa kusema wamepokea taarifa ya watu kuvamia wakiwa wamevaa sare za jeshi la polisi.

Baraza la uongozi linatoa taarifa kuwa

    Baraza limeshtushwa na kuvamiwa ofisi za Imma Advocates
    Pamoja na kuwa ni mapema, baraza linalaani uvamizi kwani unahatarisha uhuru wa sheria na mahakama.
    Kitendo cha kushambuliwa kilikuwa na lengo la kuzuia utekelezaji wa wanasheria hao.
    Kilikuwa na lengo la kuwatisha mawakili hao na wameomba niwaambie kuwa hawatotishishika.
    Kitendo hicho kinakiuka sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo nchi yetu imeingia.


Waandishi wa habari, nasema yote kwa sababu ni muhimu tukafahamu tukafahamu kazi walizokuwa wanazifanya ambazo zinaweza kuwa sababu.

    Imma wanawakilisha wateja mbalimbali, wanakilisha kampuni ya madini ya Acacia ambayo ina mgogoro mkubwa na serikali
    Inamuwakilisha katibu mkuu wa CUF
    Ni sehemu ya mawakili inayomuwakilisha anaeongea nanyi.
    Wakili wa Imma amefungua kesi dhidi ya askari aliemdhalilisha mahakamani.

Ukweli kwamba wakili Fatma ananiwakilisha katika kesi nilizo nazo mahakamani haina maana ni mwanasheria wa CHADEMA. Baada ya hayo yote tunasema nini.

Baraza la uongozi la TLS

    Linavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza haraka tukio na kupatikana kwa wahusika.
    Kuwahakishia ulinzi wa kutosha mawakili wa Imma kulingana na vitisho wanvyopata, ni wajibu wa kisheria wa serikali.
    Linawataka wanachama wote wa TLS nchi nzima kususia kuhudhuria kwa siku mbili za Jummanne na Jumatano mahakamani na kwenye mabaraza kuwaunga mkono walioshambuliwa kwa mabomu. Shambulio dhidi ya wakili mmoja linatakiwa kuwa shambulio dhidi ya mawakili wote, Imma hawatoweza kwenda mahakamani kwa siku kadhaa kwa sababu vitendea kazi vyao vimeharibiwa.
    Baraza linafanya utaratibu wa haraka kuonana na uongozi wa juu wa jeshi la polisi na usalama wa taifa kujadili kuvamiwa kwa mawakili, wawasaidie kujua nani anaewashambulia
    Linawataka wananchi kuhakikisha linalinda usalama wa mawakili ili waweze kutekeleza wajibu wao, wakitishwa watashindwa kutimiza wajibu wao wa kuwawakilisha mahakamani, tunawaomba watanzania mpaze sauti zenu.

Baada ya kusema haya, nawashukuru sana.

No comments:

Post a Comment

Popular