Diwani wa chadema: CCM inachipua chadema inakufa - KULUNZI FIKRA

Sunday 27 August 2017

Diwani wa chadema: CCM inachipua chadema inakufa

  MANENO MACHACHE NILIYOYASEMA SIKU YA MKUTANO WA SHUKRANI NA KUTAMBULISHA MADIWANI BAADA YA CHADEMA KUSHINDA NA KUUNDA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA 2015.*

    "Ndugu zangu wanachadema, wana ccm, wanachama wa vyama mbalimbali, pamoja na wananchi wote kwa ujumla.

    Ninayo kila sababu ya kumshukuru Mungu kutupa uhai, na kutufikisha siku ya leo.

    Niwashukuru ninyi nyote kwa kukiamini chama chetu na kutuamini sisi, hatimaye kaulimbiu yetu ya MSIGWA TENA NA MADIWANI mliipokea kwa moyo na kisha mmeitendea kazi kwa uaminifu, Mungu awabariki sana.

    Tumeunda HALMASHAURI, Meya na naib Meya tunao hapa pamoja na madiwani kama mnavyo tuona.

    Naomba sasa mnisikilize vizuri!

    *Kabla ya mwaka 1961 Nchi yetu ikitawaliwa na wakoloni, *TANU chini ya Mwl JK Nyerere kilionekana kuwa ni chama chenye matumaini kwa watanganyika dhidi ya unyonyaji, ghilba, ukandamizaji na uonevu na umangimeza wa serikali ya kikoloni.*

    Waliiamini TANU na Mwl Nyerere kiasi cha kuwachukia mno wakoloni, hatimaye nchi ikapata Uhuru, baadaye tumepata taifa la Tanzania, tumeendelea na TANU baadaye CCM 1977, Bila malalamiko mengi sana.

    Leo IRINGA mmeamua kutupatia tena mbunge, na zaidi sana madiwani na halmashauri, jambo zuri na la kufurahisha.

    RAI YANGU KWENU WANAIRINGA.

    Kwakuwa CHADEMA ni chama cha kisiasa na kinacho simamiwa na watu. Ninawaachia jukumu kubwa la kuwasinamia viongozi hawa hatua kwa hatua, ili kuhakikisha wanayaishi maneno yao.

    Nasisitiza tena, tusipokuwa tayari kuwafuatilia hawa viongozi wetu, *CHADEMA* hapo baadaye kinaweza kuwa chama cha hovyo.
    Sina hakika kama wenzangu mezani walikuwa wanazingatia maneno ya hotuba yangu hiyo fupi, *Bali naamini walikuwa wakifurahia kukamilika kwa mikakati miovu waliyokuwa nayo, hasa huyu mwenye chama.*

    Au pengine walikuwa wakifurahia uwepo wangu ambao walidhani unaondoa maswali kwa wananchi juu ya ushiriki wetu.

    Naikumbuka sana siku hii, kwani wakati wananchi wakiwa na furaha sana, lakini hakukuwa na furaha miongoni mwa baadhi ya madiwani na viongozi wa chama.

    Hii ilitokana na kwamba demkrasia ndani ya chama ilikuwa si tu imebakwa lakini ya mkini hata kulawitiwa kabisa(samahani kwa lugha hiyo).

    Ulikuwa ni wakati ambao hata viongozi wa chama hawakuwa na furaha kuhudhuria mkutano huo, *hata mwenyekiti wa chama hakuhudhuria japo alikuwa hapa mjini.*

    Ulikuwa ni wakati ambao Mh mwenye mamlaka ametoka kunipora kwa nguvu ushindi ambao madiwani walinipa kuwa Meya wao na kumpa amtakaye.

    Ulikuwa ni wakati ambao ametoka kututukana sana Mimi na Dady tukiwa Dodoma ya kupewa ridhaa na madiwani kuongoza HALMASHAURI, akidai kuwa hatuwezi kupewa nafasi hiyo vinginevyo CHADEMA tutagawana mbao *(nadhani alitoa unabii wa kweli kabisa bila kujua).*

    Wakati ule Mimi nilionekana mbele wa madiwani kuwa ni mkorofi sana, lakini leo kila diwani na mwanairinga anaamini nilichokisema.

    Nimeamini maneno ya MHENGA MMOJA.

    Alisema vyama ni kama mbegu.

    *Nilazima Chama kife, kioze, ndipo kichipue.*

    Kumbe wakati CHADEMA kinaanza kilikuwa ni mbegu mwenye bakuli kiking'ara sana.

    Wakati ule CCM kilishakufa, kilikuwa kimeoza, na ule usemi kwamba kimeoza ulikuwa ni wa kweli kabisa.

    Kwa sasa CHADEMA kiko kwenye stage ya kufa, na haiwezi kuchipua tena maana kiini kimeshaondolewa.

    SASA CCM BAADA YA KULE KUFA KUOZA IKO KWENYE LAST STAGE AMBAYO NI KUCHIPUA.

    Nime kuwa nasikia CCM Mpya I didn't understand how! But now my eyes are open.


    Baraka JM Kimata
    DIWANI- Kitwiru IRINGA(CHADEMA)
    

No comments:

Post a Comment

Popular