Polisi yachunguza mlipuko ofisi za wanasheria - KULUNZI FIKRA

Saturday 26 August 2017

Polisi yachunguza mlipuko ofisi za wanasheria

Kaimu kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Lucas Mkondya amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA Advocates saa  nane usiku wa kuamkia leo jumamosi , Agosti 26

Makondya amesema polisi wanafanya uchunguzi kujua ni mini kilihusika katika tukio hilo la mlipuko.
"Tupo hapa eneo la tukio,uchunguzi unaendelea na ukikamilika tutawapa taarifa zaidi, ila hatujajua kama Bomu limeusika",  amesema Makondya .
Ameelezea hadi sasa hakuna watu wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.
Mmoja wa viongozi wa kampuni ya IMMMA Advocates, Sadock Magai amesema hakuna wizi ambao umefanyika katika mali zilizokuwa ndani.
"Tuwaachie  jeshi la polisi wafanye kazi yao" amesema Magai.
Ofisi za wanasheria wa kampuni hiyo zipo barabara ya umoja wa mataifa eneo la upanga jijini Dar es salaam.
Miongoni mwa wamiliki wa kampuni hiyo Fatuma Karume ambaye ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

No comments:

Post a Comment

Popular