Mbunge wa Tunduma,Frank Mwakajoka amekamatwa na jeshi la polisi akiwa katika viwanja vya mahakama ya wilayani ya mbozi mjini vwawa.
Mwakajoka amekamatwa leo Agosti 29 baada ya kufika mahakamani hapo kwa kufuatilia kesi inayomkabili Mbunge wa mwenzake wa Mbozi,Pascal Haonga.
Katibu wa chadema wilaya ya Mbozi,James Mbasha amesema Mbunge huyo amekamatwa lakini hajui kosa linalomkabili.
Mbasha amesema amepata taarifa leo asubuhi kwamba mbunge huyo anatafutwa na polisi.
Katika kesi mahakamani hapo, Haonga na wenzake wawili Wilfred Mwalusanya na Mashaka Mwamposhi wanakabiliwa na mashtaka mawili, kufanya vurugu na kuwazui askari kufanya kazi yao kinyume na sheria.
Mwendesha mashtaka wa polisi,Samweli Saro anadai Jana,Agosti 28 saa saba mchana, washtakiwa walimzuia askari kutimiza majukumu yake ya kumkamata Masha Mwamposhi aliyedaiwa kwamba si mjumbe halali katika uchaguzi wa mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Mlawo.
Washtakiwa wanadaiwa pia kumfanyia vurugu msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mbozi,Lauteri kamao.
Washtakiwa walikana mashtaka mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo,Asha Waziri ambaye alisema dhamana iko wazi kwa kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka kwa mtendaji wa maeneo yao watakao weka bondi ya sh 2 milioni kila mmoja .
Washtakiwa walitimiza masharti na kuachiwa guru kwa dhamana,Kesi itatajwa September 25 na washtakiwa watasomewa Maelezo ya awali.
Tuesday, 29 August 2017
Home
Unlabelled
Mbunge wa Tunduma akamatwa na polisi mahakamani
Mbunge wa Tunduma akamatwa na polisi mahakamani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
No comments:
Post a Comment