Upinzani wataja mbinu mpya ya kuikosoa serikali - KULUNZI FIKRA

Tuesday 29 August 2017

Upinzani wataja mbinu mpya ya kuikosoa serikali

Viongozi wa upinzani nchini wamefunguka na kusema hakuna sababu maalum ya serikali kuwazuia kufanya mikutano ya kisiasa kwani kama ni hofu ya kukosolewa siku hizi watu hawategemei tena majukwaa wanafanya mambo kupitia hata mitandao.

Wakizungumza na kipindi cha East Africa Breafast leo asubuhi Katibu Mkuu wa Chama Cha (ADC) Doyo Hassan Doyo amesema sababu kubwa ya upinzani kutaka mikutano ya hadhara ni ili waweze kujiimarisha kwa wafuasi wake na kutangaza sera walizo nazo wala siyo kuikosoa serikali kama jinsi navyofikiriwa.

"Sisi tunahitaji mikutano ya hadhara ili tuweze kujitangaza na kuwasemea watu wetu hali zao. Mnapozungumza na watu kuhusu hali ya chama na mazingira na sera kuhusu chama chenu ndipo mahali unapoweza kujenga imani kwa wananchi kuhusu chama chako. Ni muhimu sana kujenga ukaribu kwa watu" Doyo alifunguka.

Mikutano kwetu ni muhimu kabla ya uchaguzi ili kujiweka karibu zaidi na watu wako na wakatambua pia uwepo wako. Nisehemu pia ya kufanya matangazo ya sera za chama chako na wala siyo kusema ni mahali pakukosoa kwani siku hizi unaweza hata kurekodi kitu kwenye simu au hata kwenye mitandao ya kijamii na serikali inafahamu hilo. Tusipojitangaza sasa hivi halafu ukamwambia mtu akakusikia atakuona kichekesho.

Kwa upande wa Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam Henry Kilewo amesema kuwa mikutano ya kisiasa siyo hisani ingawa ni hofu ambayo inaenezwa na maneno ya wanasiasa.
Kilewo amesema hakuna uhalali wa kuzuia demokrasia kisha ukafanya mambo mazuri kwani watu hawataona mazuri na badala yake watakuwa wanatazama kikwazo kimoja tuu ambacho ndicho wanachokitaka.

"Unajua hii mikutano siyo kama vile inavyozungumzwa. Kama ni kweli wananchi hawaitaki wairuhusu iwepo na hata ikifanyika wananchi wenyewe watachagua waende au waache" Kilewo.

No comments:

Post a Comment

Popular