Mahakama yamvua ubunge mbunge wa Longido chadema - KULUNZI FIKRA

Thursday, 31 August 2017

Mahakama yamvua ubunge mbunge wa Longido chadema

 
  Ole Nangole Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido ( chadema) ameshindwa rufaa yake ya ubunge na uchaguzi kurudiwa.

Kesi iliyofunguliwa na Mhe. Nangolo kupingwa maamuzi ya Mahakama kuu Arusha imetupiliwa mbali leo hii Mahakama ya Rufani Tanzania.

Uchaguzi unarudiwa na Maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha yanaendelea.

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido kupitia CHADEMA, Onesmo Ole Nangole alilalamikiwa na aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dk. Steven Kiruswa aliyetetewa na mawakili Dk Masumbuko Lamwai na Daud Haraka.

Mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka. Katika shauri hilo, dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni:

1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole.

2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole

3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura

4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.

5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo

No comments:

Post a Comment

Popular