Lissu ataka mawakili wasiende mahakamani siku ya Jumanne na Jumatano - KULUNZI FIKRA

Sunday 27 August 2017

Lissu ataka mawakili wasiende mahakamani siku ya Jumanne na Jumatano

Baraza la uongozi wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) limewataka mawakili nchi nzima kuto kwenda mahakamani siku ya jumanne na jumatano kama njia ya kupinga kampuni ya IMMMA Advocates kuvamiwa.
Akizungumza leo jumapili, Rais wa TLS, Mhe Tundu Lissu amesema uamuzi huo umefikiwa Jana na kikao cha baraza la uongozi la chama hicho.
Amesema mawakili wote wanaotetea wananchi kwenye mahakama na kwenye mabaraza wasifanye kazi siku hizo.
Amesema baraza hilo linafahamu kwamba Wateja wao wataathirika siku hizo lakini usalama wa mawakili ni muhimu zaidi.
Lissu amesema baraza la uongozi linavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwahakikishia ulinzi mawakili was IMMMA Advocates dhidi ya vitisho vinavyoweza kuatarisha usalama wao.
Amesema baraza hilo linafanya jitihada za kukutana na mkuu wa jeshi la polisi na Idara ya usalama ili kujadiliana kuhusu shambulio hilo.
Lissu amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda usalama, Uhuru na heshima ya wanasheria na mawakili ili waweze kutekeleza wajibu wao wa kuwatetea  wananchi.

No comments:

Post a Comment

Popular