Chama cha mapinduzi ( CCM) chafuta baadhi ya uchaguzi zake - KULUNZI FIKRA

Sunday 27 August 2017

Chama cha mapinduzi ( CCM) chafuta baadhi ya uchaguzi zake

 
 Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi, Humphrey Polepole ameongelea utaratibu wa uchaguzi ndani ya chama cha Mapinduzi ambacho kipo katika harakati za chaguzi mbali mbali ndani ya chama.

Polepole amesema uchaguzi unaendelea vizuri na unaendeshwa katika misingi ya CCM mpya, misingi akimaanisha ni kupata viongozi ambao ni waaminifu na waadilifu wakiweka maslahi ya taifa na chama mbele tayari kuwatumikia watanzania kwa nguvu zao zote.

Amesema uchaguzi wa mwaka huu ni sehemu ya mageuzi makubwa katika kukirejesha chama. Baada ya kufatilia amedai zipo changamoto, uchaguzi ukiwa sehemu ya mageuzi ndani ya chama cha mapinduzi, CCM haiko tayari kuona unahujumiwa.

CCM imetoa pongezi kwa wanachama waliofanikisha CCM mpya, lakini wapo watu wachache ambao bado hawajaelewa vizuri maana ya CCM mpya, wapo wanaoendeleza makundi katika uchaguzi kwa kupanga safu, wanaamua nani atakuwa kiongozi.

Wapo viongozi walioshindwa kutoa uangalizi mzuri kwa mali za chama cha mapinduzi lakini bado wamerejea. Kuogombea nafasi kwenye chama lazima uwe mkaazi wa eneo husika unalogombea. Wapo ambao sio wakazi na wameomba nafasi, kitu ambacho hakikubaliki, upo pia uonevu kitu ambacho hakikubaliki kwa mujibu wa CCM.

Kwa mujibu wa takwimu ambazo zitatangazwa karibuni, wanachama wa CCM wamefika milioni 12. Mwisho chama cha mapinduzi ni katiba na vikao, yapo maeneo vikao havikupewa taarifa sahihi kuhusu wagombea.

Polepole anasema anayo orodha ambayo ni awamu ya kwanza akipeleka ujumbe kwamba CCM inataka haki. Katiba yao na kanuni inasema bayana kwamba katibu mkuu wa CCM anayo mamlaka ya kutoa maelekezo ya kiuchaguzi ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika kurejesha hali ya uchaguzi.

Katibu mkuu ametoa maelekezo baada ya kupata maelekezo ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi. Chaguzi katika maeneo ambayo yatatajwa zinafutwa na zinapaswa kurejewa upya.

Polepole ametaja maeneo mengi ikiwemo kata za Buguruni, Serya.

No comments:

Post a Comment

Popular