Rais Magufuli afuta chaguzi katika kata 25. - KULUNZI FIKRA

Sunday 27 August 2017

Rais Magufuli afuta chaguzi katika kata 25.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ( CCM), Rais John Maguful, ameagiza kufutwa kwa chaguzi katika kata 25 nchini kutokana na dosari zilizotokea ikiwa pamoja na kuingiliwa na makundi ya wagombea Urais wa mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Jana jumapili,katibu wa Itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole alisema pamoja na sababu hiyo, baadhi ya viongozi wa kata wameshindwa kutoa Maelezo ya usimamizi wa mali za chama.
"Mwenyekiti wetu Rais Magufuli pamoja na katibu mkuu Abdulrahman Kinana walipokea malalamiko ya wanachama na kuyatafakari na kuchukua hatua hiyo," Alisema Polepole.

No comments:

Post a Comment

Popular