Kamanda Mambosasa: Katika kipindi changu hakuna askari kumkamata mtu kwa order kutoka juu - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 29 August 2017

Kamanda Mambosasa: Katika kipindi changu hakuna askari kumkamata mtu kwa order kutoka juu

 
 => SACP Lazaro Mambosasa aahidi kushirikiana na wananchi katika uongozi wake ili kuiweka Dar es Salaam salama dhidi ya uhalifu.

    => Ukisikia askari anasema 'order' kutoka juu ujue huyo hajiamini na pengine ni mbabaishaji hajui anachotenda.

    => Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa kuzingatia katiba,sheria,kanuni na miongozo inayoliongoza Jeshi la polisi.

    => Katika kipindi changu hutasikia kauli ya 'order' kutoka juu na ukisikia ikatie rufaa, nipigie niambie

    Kamanda mpya wa mkoa wa Dar Lazaro Mambosasa amejitambulisha kwa waandishi wa habari leo

    Moja ya maswali ambayo ameulizwa na waandishi wa habari ni juu ya watu kukamatwa hovyo na polisi kwa kile kinachosemekana ni ''amri kutoka juu'' Kamanda Mambosasa alijibu swali hilo kwa kutoa maelezo haya

    ''Katika kipindi changu hutasikia kauli ya 'order' kutoka juu na ukisikia ikatie rufaa, nipigie niambie kuna mtu anataka kuchezea uhuru wangu, Ukisikia askari anasema 'order' kutoka juu ujue huyo hajiamini na pengine ni mbabaishaji hajui anachotenda. Jeshi la Polisi linafanyakazi kwa kuzingatia katiba,sheria,kanuni na miongozo inayoliongoza Jeshi la polisi”

    Nguvu ya kumkamata mtu tunaipata kwenye kifungu namba 14 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kama ilivyopitiwa mwaka 2002''

    ''Hakuna kosa ambalo mtu anakamatwa halafu isiangukie kwenye sheria hiyo halafu akasema imetoka juu labda angesema anakukamata siokwa amri ya polisi lakini kuna amri ya mahakama, kuna arrest warrant imetolewa, ambayo inataka wewe ukamatwe umeshtakiwa Simiyu tunataka tukusafirishe kwenda huko lazima kuwe na maelezo toshelevu.

    Katika kipindi changu ukisikia mtu anakukamata kwa kauli hiyo nipigie uniambie kuna mtu anachezea uhuru wangu''
    

No comments:

Post a Comment

Popular