Korea kaskazini yarusha makombora baharini karibu na kisiwa cha Hokkaido nchini Japan, Waziri mkuu ang' aka. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 29 August 2017

Korea kaskazini yarusha makombora baharini karibu na kisiwa cha Hokkaido nchini Japan, Waziri mkuu ang' aka.

 
 Korea kaskazini imerusha makombora yake ambayo yalipita Japan kabla ya kudondokea baharini.
Makombora hayo yalisafiri kuelekea mashariki karibu kilomita elfu moja juu ya kisiwa cha Japan cha Hokkaido.

Tukio hilo limechochea tahadhari ya hatari ambayo watu walielekezwa kujificha katika maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyo imara.

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake.

Katika mfululizo wa majaribio yake ya makombora ya hivi karibuni Korea kaskazini haijawahi kurusha makombora yaliyopita juu ya ardhi ya nchi hiyo, hivyo tukio hili la sasa limeleta wasiwasi mkubwa.

Katika siku za hivi karibuni Pyongyang ilijaribu kombora lake lililopata mafanikio kutokana na uwezo wake wa kuweza kuifikia Marekani na kuonyoa kuwa inasimamia mipango yake ya kushambulia kwa makombora eneo la Marekani la Guam, kilomita elfu mbiili kusini mashariki mwa Japan.

No comments:

Post a Comment

Popular