Hospital ya kairuki yakanusha tuhuma za mgonjwa kuachwa kwa vifaa vya kuzalishia - KULUNZI FIKRA

Tuesday 29 August 2017

Hospital ya kairuki yakanusha tuhuma za mgonjwa kuachwa kwa vifaa vya kuzalishia

 
 TAARIFA KWA UMMA KUKANUSHA TUHUMA ZA MGONJWA KUACHWA NA VIFAA VYA KUZALISHIA UKENI​

Uongozi wa Kairuki Hospital umepokea na kusoma kwa masikitiko taarifa zilizoandikwa na magazeti ya tarehe 28/8/2017 pamoja na kusambazwa kwenye rnitandao mbalimbali ya kijamii kuwa hospitali yetu imemsababishia mgonjwa madhara ya kizazi kwa kurnuacha na vifaa vya kuzalishia ukeni.

Magazeti yaliyotufikia yakiwa na tuhuma hizo ni pamoja na gazeti la Uhuru toleo na. 22847, Mtanzania toleo Na. 8651 pamoja na Daily News lenye toleo Na. 12021 yote yakiwa ya tarehe tajwa hapo juu.

UKWELI KUHUSU MGONJWA ANAYETAJWA
Hospitali inakiri kuwa iliwahi kumhudumia mama mjamzito aitwaye Khairat Shaib Omary mkazi wa Mbezi Beach Dar es Salaam mnamo mwaka 2016. Mama huyo alihudumiwa kwa muda wa ujauzito wake kwa nyakati tofauti alizofika hospitalini kwetu. Pia alihudumiwa kwa kupewa huduma za kujifungua ambapo tarehe 15/12/2016 alijifungua kwa njia ya upasuaji baada ya njia za kawaida kushindikana kwa sababu zisizozuilika kitabibu. Mnamo tarehe 17/12/2016 mama huyo na mtoto wake waliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya madaktari wetu kuridhika kuwa afya ya mama na mtoto zilikuwa salama na wakiendelea vizuri.
Mama huyo alirejea tena hospitalini kwetu tarehe 21/12/2016 kwa ukaguzi wa kawaida baada ya kujifungua ambapo daktari aliyemhudumia aliridhika kuwa afya ya mama huyo ilikuwa salama na hakuwa na tatizo lolote kwani hata kidonda cha mshono wake kilikuwa kikiendelea kupona vizuri. Mama huyo hakurejea tena hospitalini hapo kwa matibabu wala huduma zaidi ya hapo mpaka leo.

TUHUMA KUHUSU KUACHWA NA VIFAA VYA KUZALISHIA UKENI
Kwa mara ya kwanza, tuhuma kuhusu mgonjwa aitwaye Khairat Shaib Omary, ziliwasilishwa kwetu mnamo tarehe 10/7/2017 kufuatia barua ya wakili wake aitwaye Jonas Estomih Nkya wa kampuni ya Jonas & Associates Law Chambers ambaye alitutaka tumlipe mteja wake Milioni mia Sita (Tshs.600,000,000/=) pamoja na riba ya asilimia ishirini na moja (21%). Hospitali yetu ilikanusha

kuhusika na tuhuma na madai ya Bi. Khairat Shaib Omary ambaye aliamua kufikisha madai yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu katika kesi Namba 184 ya mwaka 2017 akidai fidia mbalimbali.

Wakati kesi hiyo ikiwa .tayari imepangiwa Hakimu wa kuisikiliza pamoja na tarehe ya kuitaja mahakamani, mgonjwa huyo ameendelea kutumia vyombo vya habari kutuchafua kwa nia ambayo sisi tunaamini ni kutaka kushinikiza hukumu yenye upendeleo kutoka mahakamani kitendo ambacho hakikubaliki kamwe.

Hospitali yetu inapenda Umma ufahamu kuwa baada ya tarehe 21/12/2016, Bi Khairat Shaib Omary, anakiri katika hati zake za madai, kuwa alihudumiwa katika hospital nyingine tofauti kama vile Tanzania Occupational Health Services, Regency Hospital na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa nyakati tofauti. Hata hivyo, hakuwahi kutaarifu hospitali yetu kuhusu huduma alizopewa kwenye hospitali hizo.

Hospitali inakanusha tuhuma zilizoandikwa na magazeti tajwa hapo juu kwa kuwa hazina ukweli wowote. Endapo mgonjwa anayetajwa na magazeti anayo madai ya msingi dhidi ya Kairuki Hospital, alitakiwa kusubiri taratibu za Mahakama alizokwishazianzisha iii alete ushahidi na kuthibitisha tuhuma zake.

Kairuki Hospital tunasikitika kuona vyombo vya habari tajwa hapo juu vikiandika habari za kututuhumu bila kutuhoji wala kutupatia fursa ya kueleza nafasi yetu na nini kilifanyika kuhusu mgonjwa huyo. Kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki zetu za msingi pamoja na maadili ya wanahabari.

Kairuki Hospital tunataka Umma, wateja wetu, wadau na wafanyakazi wote kuwa wazipuuze tuhuma zinazoendelea kuandikwa kwenye magazeti na mitandao ya kijamii kuhusu kuacha vifaa vya kuzalishia kwenye uke wa mgonjwa kwani hazina ukweli. Aidha, tunasikitika kwa usumbufu ambao umeshajitokeza kufuatia taarifa hizo.

Kwa sasa, Kairuki Hospital ipo katika mchakato wa kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha haki inatendeka kwa upande wetu na kukomesha vitendo vya wanahabari kutuhumu bila kupata maoni na taarifa sahihi za upande wa pili.


Imetolewa leo tarehe 28/8/2017.


Arafa Juba


Afisa Habari


KAIRUKI HOSPITAL

No comments:

Post a Comment

Popular