Ajari kisarawe: Gari lapinduka baada ya kuacha njia na kuua baba na mwana - KULUNZI FIKRA

Monday, 28 August 2017

Ajari kisarawe: Gari lapinduka baada ya kuacha njia na kuua baba na mwana

 Mtoto wa miaka miwili amefariki dunia na watu wengine watano wamejeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Land Cruiser walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Kibuta wilayani Kisarawe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shana, amesema ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Agosti 28.

Amemtaja mtoto aliyefariki katika ajali hiyo kuwa ni Muslimu Ibrahimu na miongoni mwa majeruhi ni dereva Omary Kamungu, ambaye ni ofisa maendeleo ya jamii mkoani Mbeya.

Dereva huyo anashikiliwa na Polisi kwa ajili ya mahojiano.

Kamanda Shana amesema majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambako wamelazwa wakipatiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment

Popular