Viwanja zaidi ya 22,000 na hoteli za kifahari katika Manispaa ya Dodoma zinatarajiwa kuondolewa ili kupisha makazi ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hali hiyo inakuja ikiwa ni miezi 11 tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipohamia rasmi mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi alisema jana kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuboresha mji huo ambao kwa sasa umebeba jukumu la makao makuu.
Alisema mpango wa kuzivunja hoteli hizo ni kawaida kwa kuwa hawawezi kuruhusu zikaendelea wakati zipo karibu na makazi ya Waziri Mkuu eneo la Mlimwa.
Hoteli zilizopo karibu na makazi hayo ni African Dream, Royal na nyingine mpya.
Pia, Kunambi alitoa nafasi ya mwezi mmoja watu waliopewa barua za viwanja wawe wamekamilisha kuvilipia kabla ya maeneo hayo kutwaliwa.
Naibu Meya wa Manispaa, Jumanne Ngede, alisema mipango ya sasa ndani ya Manispaa hiyo ni tofauti na zamani hivyo wanaweza kuamua jambo na kulitekeleza mara moja.
Ndede alisema kuondolewa kwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) kumeiwezesha manispaa kuvunja lengo la makusanyo ya ndani kutoka Sh 3.9 bilioni walizolenga hadi kufikia Sh4. 6 bilioni.
Alisema mwaka wa fedha 2017/18 wanatarajia kukusanya zaidi ya kiwango hicho.
Mkazi wa Manispaa ya Dodoma, Rehema Yobwa, alisema mikakati inayowekwa na kutekelezwa na viongozi hao, inashindwa kutofautisha kati ya CDA na Manispaa katika masuala mazima ya ardhi.
Tuesday, 29 August 2017
Home
Unlabelled
Dodoma: Viwanja 22,000 na hoteli za kifahari kuvunjwa kupisha makazi ya ofisi ya Waziri mkuu
Dodoma: Viwanja 22,000 na hoteli za kifahari kuvunjwa kupisha makazi ya ofisi ya Waziri mkuu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Vat leaching gold processing method is the recently technology that practised in developing nations. In Tanzania vat leaching method w...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
No comments:
Post a Comment