Dar es Salaam. Chama Cha Wananchi (Cuf) kimetoa pole baada ya ofisi Mawakili wa Kampuni ya Ishengoma Karume Masha and Magai (IMMMA ADVOCATES) yenye makao makuu yake kando ya barabara ya Umoja wa Mataifa, Upanga, Dar es Salaam kuteketea kwa moto.
Chama hicho kimedai kupokea kwa masikitiko ya taarifa ya kutokea kwa moto ulioteketeza ofisi hizo leo asubuhi.
Pole hiyo imetolewa kupitia taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Habari uenezi na Mahusiano ya Umma Mbarala Maharagande kwa madi kwamba kwamba kinatambua mchango wao katika kupigania haki.
“Tunatoa pole na kuungana na Mawakili na wafanyakazi wote katika kipindi hiki kigumu cha uharibfu wa mali na vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani kubwa. Tunatambua mchango mkubwa wa Kampuni ya IMMMA na mawakili wake katika kutetea na kupigania haki, usawa, demokrasia na utawala bora katika nchi yetu,” amesema Maharagande.
Chama hicho kililitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka katika kufanyia uchunguzi tukio hilo na kutoa taarifa kwa umma ili ujue nini chanzo cha moto huo.
“Nchi yetu hivi sasa imekumbwa na matukio makubwa ya ukiukwaji wa haki za binaadamu na vitendo vya uhalifu vinavyoonekana wazi kuwa vinaratibiwa makhsusi na kikundi cha watu wenye nia ovu dhidi ya watetezi wa haki, uhuru na demokrasia kwa lengo la kuogofya,” anasema.
Amesema ni wajibu na jukumu la kila Mtanzania kupinga na kulaani vitendo na mwenendo mbaya wa muelekeo wa Taifa letu katika hali hii.
Saturday, 26 August 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...
No comments:
Post a Comment