Libya yamkamata jasusi wa Massod Aliyekuwa kiongozi wa kidini - KULUNZI FIKRA

Sunday 27 August 2017

Libya yamkamata jasusi wa Massod Aliyekuwa kiongozi wa kidini

 
 Maafisa wa Libya wamethibitisha kuwa, wamemtia nguvuni kiongozi wa kundi la Daesh ambaye alikuwa akilifanyia kazi shirika la ujasusi la Israel, Mossad.
Maafisa wa Libya wamesema kuwa, Myahudi huyo aliyejulikana kwa jina la "Abu Hafs" alikuwa imamu wa jamaa wa msikiti mmoja katika mji wa Benghazi na kwamba baada ya uchunguzi imebainika kuwa, ni raia wa Israel na jina lake halisi ni Benjamin Efraim.    Maafisa wa serikali ya Libya wameongeza kuwa, Efraim alikuwa akikifanyia kazi kikosi cha Mossad cha Wayahudi waliojifanya Waarabu na kufanya ujasusi katika nchi za Kiarabu na Kiislamu kwa maslahi ya Israel. Wameongeza kuwa, jasusi huyo alikuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la Daesh na aliweza kuhamia katika mji wa Benghazi kupitia kwa kundi hilo na kuwa imamu wa Swala za jamaa.

"Abu Hafs" yaani Benjamin Efraim, alikuwa kiongozi wa wapiganaji 200 wa kundi la kigaidi la Daesh ambao wanatambuliwa kuwa makatili zaidi kuliko magaidi wengine wa kundi hilo.
Maafisa wa serikali ya Libya wanasema, lengo la kundi hilo lilikuwa kupata ushawishi na badaye kuhamishia vita na mapigano katika nchi jirani ya Misri.

No comments:

Post a Comment

Popular