Wabunge na madiwani hao wanaomuunga mkono katibu mkuu wa cuf,Self Sharif Hamad waliitwa ili kuojiwa na kamati nidhamu na maadili ya chama hicho kuhusu mgogoro unaoendelea.
Katika taarifa iliyotolewa juzi na chama hicho na upande unaomuunga mkono mwenyekiti profesa Ibrahim Lipumba uliwataka viongozi hao kufika katika ofisi hizo saa 3:00 asubuhi jana.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti,mbunge wa viti maalum wa chama hicho aliyeitwa kwenye mahojiano hayo,Severina Mwijage amesema hana taarifa zankuitwa kwenye kikao hicho.
"Niko safarini Bukoba sifahamu kuwepo kwa kikao hicho", Amesema.
Mbunge mwingine wa viti maalum wa chama hicho,Mgeni Kadika alisema alipata taarifa za kuwepo kwa kikao hicho lakini hata hudhuria.
" Nilipata taarifa kupitia ujumbe mfupi(SMS) lakini sitafika kwenye kikao hicho kwa kuwa nauguliwa na watoto huku Pemba",Amesema.
No comments:
Post a Comment