Kafulila amepokea pongezi za Rais Magufuri kwa mikono miwili - KULUNZI FIKRA

Monday, 24 July 2017

Kafulila amepokea pongezi za Rais Magufuri kwa mikono miwili

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia Chama Cha NCCR-Mageuzi, ambaye sasa ni Mwanachama wa Chadema, DAVID KAFULILA, amesema kauli ya Rais JOHN MAGUFULI ya kumpongeza kwa juhudi zake za kuibua Bungeni Kashfa ya Tegeta Escrow, ameipokea kwa Moyo mmoja kwa kuwa Imemgusa na Kumfariji.

Akizungumza na Uhuru FM, KAFULILA, amesisitiza kuwa vita dhidi ya Wahujumu Uchumi haina Chama, hivyo Wanasiasa hususani Vijana wanatakiwa kumuunga mkono Rais, katika vita hiyo ya Kiuchumi ambayo ameianzisha.

Amesema anampongeza kwa dhati Rais, MAGUFULI kwa kumpongeza hadharani kutokana na kutambua mchango wake katika kupigania rasilimali za nchi.

KAFULILA amefafanua kuwa Vita dhidi ya Uchotwaji wa Mabilioni ya Fedha ya Akaunti ya Tegeta Escrow aliyoiibua katika Bunge la Bajeti mwaka 2013, haikuwa rahisi, kwani ilimtesa ndani na nje ya Jimbo lake kutokana na kupigwa Vita na baadhi ya Wabunge.

Jana katika mkutano wa hadhara, Rais MAGUFULI, akiwa Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, amemsifia, KAFULILA, huku akisema Kijana huyo ni Mzalendo kwa kuwa alisimama Imara kupigania Masilahi ya Umma.

No comments:

Post a Comment

Popular