Mkazi wa ubungo jijini Dar es salaam, amenusurika kifo baada ya ya kupigwa risasi wakati akitaka kuingia katika kanisa katoliki,parokia kibangu,wilayani ubungo.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi kinondoni,Suzan Kaganda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Akisimulia tukio hilo mfanyakazi wa kanisa hilo,George Ng'atigwa amesema aliyejeruhiwa ni muumini wa kanisa hilo aliyemtaja kwa Nina la Adrian Mpunde.
Amesema tuki hilo lilitokea majira ya saa 3 asubuhi wakati muumini Hugo alikuwa nje ya kanisa akisubiri muda ufike ili aingie kanisani.
"Mara akatokea mtu mwenye bastora akampiga risasi ya ubavuni na mkononi akaanguka na kuzimia", amesema.
Amesema baada ya kutekeleza unyama huo,mtu huyo ambaye aligika kanisani halo akitembea kwa miguu,alikimbia.
Inaonekana alikamatwa baada ya bastora yake kuishiwa risasi kwa kuwa wakati anakimbia hakuwa akiwatisha waliokuwa wakimfukuza",amesema.
Amesema baada ya kukamatwa, walifanya mawasiliano na polisi ambao walifika baada ya muda na kuondoka naye.
Alisema aliyejehiwa kwa risasi alipata Huduma ya kwanza katika zahanati iliyopo jirani na kanisa hilo na baadae kupelekwa katika hospitali ya Taifa muhimbili.
Akifafanua,kamanda wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni,Kaganda alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba ni ugomvi wa kifamilia.
"Mtuhumiwa tunaye tunaendelea kumhoji na aliyepigwa risasi anaendelea vizuri na matibabu katika hospitali yaTaifa muhimbili", Amesema.
Sunday, 23 July 2017
Home
Unlabelled
Apigwa risasi nje ya kanisa kibagu jiji Dar es salaam
Apigwa risasi nje ya kanisa kibagu jiji Dar es salaam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
-
Tanzania imechanua na kufanya vizuri katika viwango vilivyotolewa na mfuko wa Mo Ibrahim uliopima hali ya utawala bora na maendeleo na ku...
No comments:
Post a Comment