JPM ampongeza kafulila kwa kuibua sakata la IPTL - KULUNZI FIKRA

Sunday, 23 July 2017

JPM ampongeza kafulila kwa kuibua sakata la IPTL

Rais John Pombe Magufuri amempongeza  Aliyekuwa mbunge wa kigoma kusini,David kafulila kwa kuibua sakata la mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuelezea waliombeza na kumuita tumbili watakuwa tumbili wao.
Akiwa anahutubia wananchi wa Nguruka wilaya ya uvinza mkoani kigoma, Rais Magufuri akisema "kabla  sijamaliza napenda kumpongeza Kafulila ambaye alijitolea kuibua sakata la IPTL,na wengine wakamuita tumbili kwa kubeza sasa wao ndio watakuwa tumbili", amesema
Magufuri amesema" Aliyemuita kafulila tumbili yeye ndiye tumbili, kafulila katetee wanyonge hadi wakudhihaki,ila wao ndio tumbili wewe ni mtu safi".
Akiwa bungeni mwaka 2014,Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali (AG), Jaji Frederick Werema alizua tafrani akiwa bungeni kutokana na kitendo chake cha kutaka kumpiga mbunge wa kigoma kusini, kafulila wakati huo akiwa NCCR-Mageuzi.
Sakata hilo lilitokea baada yabaada ya mwenyekiti wa bunge, Mussa Azzan Zungu kuahirisha kikao cha Bunge, Ikiwa ni muda mfupi baada ya Werema na kafulila kurushiana maneno bungeni ambapo jaji Werema alichukia baada ya kafulila kumuita mwizi

No comments:

Post a Comment

Popular