Tundu Lissu amesomewa mashtaka ya uchochezi - KULUNZI FIKRA

Monday, 24 July 2017

Tundu Lissu amesomewa mashtaka ya uchochezi

Mwanasheria mkuu wa chadema, Tundu Lissu amefikishwa katika mahakama ya kisutu Der es salaam na kusomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi.Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu mkazi mkuu wa,Wilbard Mashauri Leo Jumatatu julai 24,mahakama imeelezeawa kuwa Lissu ametoa lugha ya uchochezi dhidi ya serikali julai 17 akiwa maeneo ya ufipa kinondoni.
Imedaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo la kuleta chuki dhidi ya serikali ya jamhuri UA muungano wa Tanzania.
Alipotakiwa kukubali ama kukuataa makosa hayo na Hakimu Mashauri,Lissu amesema kusema ukweli haijawahi kuwa kosa la jinai.
Kwa sasa upande wa mashtaka wameomba Lissu anyimwe dhamana na upande wa uteyezi wanaopinga hoja ambazo zinaendelea.

No comments:

Post a Comment

Popular