Cuf yatangaza kuwavua uwanachama wabunge nane - KULUNZI FIKRA

Monday, 24 July 2017

Cuf yatangaza kuwavua uwanachama wabunge nane

Baraza kuu la uongozi la Taifa la chama cha wananchi (CUF) limewavua uanachama wabunge name wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu,yakiwamo kukisaliti chama hicho.
Mwenyekiti wa CUF,anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa,profesa Ibrahim Lipumba amesema,baraza pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalum wa mkoa wa Dar es salaam kwa makosa hayo.
Profesa Lipumba ametangaza uamuzi huo Leo jumatatu,julai 24 wakati wa mkutano wake na wanahabari uliofanyika makao makuu ya CUF,Buguruni ,Dar es salaam.
"Leo asubuhi tumewasilisha nyaraka za hatua hizi kwa sipika na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwa hatua zaidi," amesema profesa Lipumba.
Amesema wabunge hao nane ni kati ya kumi walioitwa hivi karibuni na kamati ya maadili na nidhamu kwa mahojiano wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa Maelezo kuwa walitaka kushikiana na chadema kumwondoa yeye madaraka.

No comments:

Post a Comment

Popular