Tume ya vyuo vikuu Tanzania imetangaza kusitisha udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18 kwa vyuo vikuu 19 nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu mtendaji wa Tume hiyo, Prof. Eleuther Mwageni, uamuzi huo unatokana na matokeo ya uhakiki ilioufanya mwezi Septemba na Oktoba mwaka 20i6.
Taarifa hiyo imesema kuwa lengo la uhakiki huo ilikuwa ni kuhakiki ubora wa elimu inayotolewa vyuoni, ambapo ripoti yake imebainisha upungufu kadhaa katika baadhi ya vyuo vikiwemo vyuo hivyo, lakini haikuweka hadharani ni aina gani ya upungufu uliobainika.
Prof. Mwageni katika taarifa hiyo amevitaja vyuo vilivyositishiwa udahili kuwa ni pamoja na
Eckenforde Tanga University
Jomo Kenyatta University, Arusha
Kenyatta University, Arusha
United African University of Tanzania
International Medical and Technological University (IMTU)
University of Bagamoyo
Francis University College of Health and Allied Sciences
Archibishop James University College
Archibishop Mihayo University College
Cardinal Rugambwa Memorial University College
Kampala International University Dsm College
Marian University College
Johns University of Tanzania Msalato Centre
Johns University of Tanzania, Marks Centre
Joseph University College of Engineering and Technology
Teofilo Kisanji University
Teofilo Kisanji University Tabora Centre
Tumaini University, Mbeya Centre
Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMCo)
Mbali na kusitisha udahili katika vyuo hivyo, pia TCU imesitisha jumla ya programu 75 kutoka vyuo 22 nchini kutokana na upungufu katika vyuo hivyo.
Aidha, tume hiyo imesema uamuzi huo hautawahusu wanafunzi wanaondelea na masomo katika programu na vyuo husika.
Tuesday, 25 July 2017
Home
Unlabelled
TCU yafungia vyuo 19 zisivyo na sifa ya kudahili mwaka huu
TCU yafungia vyuo 19 zisivyo na sifa ya kudahili mwaka huu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
-
Tanzania imechanua na kufanya vizuri katika viwango vilivyotolewa na mfuko wa Mo Ibrahim uliopima hali ya utawala bora na maendeleo na ku...
No comments:
Post a Comment