spika wa bunge,Job athibitisha kupokea barua ya kuvuliwa uanachama wabunge 8wa cuf - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 25 July 2017

spika wa bunge,Job athibitisha kupokea barua ya kuvuliwa uanachama wabunge 8wa cuf

Mhe. Spika amepokea barua kutoka kwa kwa mhe Ibrahim Lipumba mwenyekiti wa Taiga wa chama cha wananchi (CUF) na mhe Magdalena Sakaya(MB) na kaimu katibu mkuu (CUF)ambapo wamemuarifu kuhusu uamuzi wa baraza kuu la chama hicho kuwafukuza wabunge wanane na madiwani wawili kwa makosa kadhaa ya nidhamu.
Katika barua hiyo ,viongozi hao wametaja wanachama hao ambao ni wabunge kuwa ni
         (1) Mhe.Severina Silvanus Mwijage (MB)
         (2)Mhe.Saumu Hero Samara(MB)
         (3)Mhe.Salma Mohammed Mwassa(MB)
         (4)Mhe.Riziki Shahara Ngwari(MB)
         (5)Mhe.Rais Abdallah Mussa(MB)
         (6)Mhe.Miza Bakari Haji(MB)
         (7)Mhe.Hadija Salum Ally(MB)
         (8)Mhe.Halima Ali Mohammed (MB)
Aidha,barua hiyo imeainisha makosa yao kuwa ni kukiuka kifungu cha 83 (4)na (5) cha katiba ya chama hicho.
Mhe.spika amepokea barua hiyo na kutoa rai kwa umma kuwa,swala la kuwaondoa uanachama ni la utashi wa vyama vyenyewe na kila chama kina utaratibu wake wake,hivyo bado naendelea kuitafakari barua hii na taarifa rasmi kuhusu maamuzi ya spika kwa wabunge waliofukuzwa nitayatoa hapo baadae",amesema.

No comments:

Post a Comment

Popular