Golikipa wa Timu ya Taifa ya vijana wenye chini ya miaka 17 'Serengeti Boys', Ramadhani Kabwili, amejiunga rasmi na Yanga kwa mkataba wa miaka mitano.
Kipa huyo ambaye hakuwa na timu yoyote kabla ya kujiunga Yanga, ni miongoni mwa vijana waliochukuliwa wakiwa bado shuleni na kupata mafunzo katika kituo cha vipaji cha TFF, (TSA) Karume jijini Dar es salaam.
Kabwili ameiongoza Serengeti Boys katika michuano ya AFCON kwa vijana iliyofanyika mwezi Mei mwaka huu nchini Gabon akiruhusu mabao mawili pekee katika mechi tatu ambazo Serengeti Boys ilizocheza licha kutupwa nje ya michuano hiyo kwa sheria ya ‘head-to-head’ baada ya kufungwa 1-0 na Niger.
Kabwili pia alikuwa na mchango mkubwa katika kuiwezesha Serengeti Boys kufuzu hatua michuano hiyo kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika mechi za awali za kufuzu pamoja na mechi kadhaa za kirafiki.
Kwa kumpa mkataba wa miaka mitano tofauti na wachezaji wengine ambao hupewa mikataba ya miaka miwili pekee ni wazi kuwa klabu hiyo ina malengo ya muda mrefu na kinda huyo ambaye bado hajafikisha umri wa miaka 18.
Usajili huo unakamilisha idadi ya makipa watatu klabuni hapo, ambapo wengine ni Deogratius Munis ‘Dida’ pamoja na Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon.
Tuesday, 25 July 2017
Home
Unlabelled
Kipa wa Serengeti Boys anasa Yanga miaka mitano
Kipa wa Serengeti Boys anasa Yanga miaka mitano
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
-
Tanzania imechanua na kufanya vizuri katika viwango vilivyotolewa na mfuko wa Mo Ibrahim uliopima hali ya utawala bora na maendeleo na ku...
No comments:
Post a Comment