Ripoti LHRC yabaini ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. - KULUNZI FIKRA

Monday, 31 July 2017

Ripoti LHRC yabaini ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Ripoti ya nusu mwaka ya haki za binadamu ilizinduliwa Leo jumatatu na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) inaonyesha bado hali sio nzuri nchini.
Akizindua ripoti hiyo Leo jijini dar es salaam,mkurugenzi wa LHRC Dkt Haleni kijo-Bisimba amesema inaonyesha kuna ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi kutokana na watu wengine kuuawa kwa sababu mbalimbali.
Amesema katika kipindi cha kuanzia January hadi June ,watu kadhaa wameuawa kwa sababu mbalimbali, ikiwamo tuhuma za ushirikina na watu kujichukulia sheria mkononi .
"Watu 115 wameuawa wakituhumiwa ni washirikina ,kati ya vifo hivyo 23 vimetokea mkoani Tabora ambao unaongoza,ukifuatiwa na kigoma wenye vifo 23 na Kagera 11"'amesema Dkt kijo Bisimba .
Amesema matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi nayo yamerudi kwa kazi kwani taarifa za polisi zinaonyesha kuwa  watu 479 wameuawa na wananchi wenye hasira Kali .
Mkoa wa Dar es salaam ndiyo unaongoza kwa matukio hayo kwa kuwa na vifo 117,ukifuatiwa na Mbeya vifo 33, Mara 28 na Geita 26.
"Taarifa ya kipindi hiki inaonyeshwa ukiukwaji mkubwa wa haki za raia hususani haki ya kuishi, lakini pia ukiukwaji mkubwa wa haki za makundi maalum hasa wanawake na watoto," amesema.
Pia amesema kuna vifo Tisa ambavyo vinahusisha vyombo vya dola, ingawa jeshi la polisi katika taarifa yake inayoonyesha ni mtu mmoja pekee ndiye aliuawa mikononi mwao.

No comments:

Post a Comment

Popular