Leo kuna mkutano wa chadema na wanahabari unaofanyika upanga kwenye hotel ya courtyard protea .
Huu mkutano wa uongozi wa juu wa chama na wahariri pamoja na waandishi wa habari waandamizi, umeanza toka saa 04:30 asubuhi,katika hostel ya protea courtyard
Hii inatokana na uamuzi ambao kamati kuu ya chadema,mkutano wa kamati kuu ya chadema uliofanyika katika hostel ya Double Tree jijini Dar es salaam.
Maeneo ambayo yamejadiliwa na kuridhia kuchukuliwa kwa hatua ni
(1)Hali ya mwenendo wa siasa katika nchi na ukandamizaji wa demokrasia unaofanywa na serikali ya awamu ya tano
(2)Kuporomoka kwa uchumi na halia ngumu ya maisha kwa watanzania.
(3) Kamata kamata inayoendelea kwa kufanya na vyombo vya dola dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa chadema maeneo mbalimbali nchi mzima
Mbowe: Kamati kuu ilikua na kikao cha siku mbili kilichoranguliwa na Mkutano maalum
=>Viongozi wakuu walijumuika na Viongozi wa kanda mbalimbali za chadema
=>Tulitafakari kwa kina hali za kisiasa na kamatakamata kwa viongozi wa Upinzani na hali ya Uchumi wa taifa
=>Kikao cha leo kitajadili jambo moja. Hali ya uchumi katika taifa
=>Tumezoea kuzungumza maswala ya kisiasa, lakini sisi kama taifa hatujanipa nafasi ya kutambua hali ya uchumu.
=>Rais wetu tumempa likizo sana sababu yeye na serikali yake hawajabanwa vizuri kuhusu hali ya uchumi
=>Vyombo vyetu vimekua vikiangalia uchumi kutokana na kauli za Serikali, sio mbaya. Lakini inatakiwa tujue hali hii inatupeleka wapi.
=>Bank ya dunia huo inatoa taarifa IMF na BOT. Mtu anayetoa taarifa halisi ni bank kuu. Na leo tutatumia taarifa za Bank kuu.
=>Kila mwezi bank kuu inatoa taarifa ya kiuchumi
=>Sababu ya faida ya kikao hiki ntazungumzia mambo madogo sita
=>May 2015- may 2017 ni mambo gani yanaendelea katika nchi
=>Wataalam wetu wamefanya uchunguzi wa kinachosababisha uchumi kuporomoka.
=>Nianze na jambo la kwanza: Chakula
=>Chakula ndo maisha yetu. 75% ni wakulina katika nchi yetu
=>Chakula ndo maisha yetu. 75% ni wakulina katika nchi yetu
=>Rais anasema hatatoa chakula "Magufuli, hiki chakula si chako"
=>Serikali ya awamu ya nne 2015 tulikuwa na tani zaidi ya laki nne. Lakini 2017 kuna tani 74 elfu ambayo ni Asilimia 18 ya chakula ukilinganisha na awamu ya nne
=>Vyakula vyote sasa vimepanda bei wakati mapato kwa wananchi yanashuka. Mishahara haijaongezwa wala rais halimsumbui hilo
=> Sekta ya kilimo imekuwa kwa 1.7% tangu Rais aingie madarakani
=>Wakati mataifa mengine yanasaidia nchi zao kupata chakula sisi hatufanyi hivyo
=>Tume ya maji ya kuboresha kilimo cha umwagiliaji haijapewa kitu
=>Uchumi unakuwa kwenye mifuko ya watu wachache. Uchumi unakuwa wakati umasikini unaongezeka.
=>Sekta ya Kilimo ufugaji na uvuvi inasinyaa
=>Kipaumbele cha rais ni kununua ndege. Hii fedha ya ndege ingepelekwa kwenye kilimo, watanzania mil40 wangecheka.
HALI YA UKATA WA NCHI
=>Ukata unasababishwa na usimamizi mbovu wa Uchumi. Mzunguko wa fedha umeathirika sana
=> Fedha iliyoingizwa kwenye mzunguko imepungua kwa asilimia tano. Hali hii inasababisha mdororo wa uchumi.
=>Sekta binafsi ndo sekta inaongeza uchumi wa taifa. Rais anaamini kila mmoja kwenye sekta binafsi ni mpiga dili. Rais bado anaamini anaweza kurudisha hili taifa kwenye ujamaa
=> Kuna ugonjwa ambao ukiusikia kama unajua biashara utajiuliza hivi sisi tuna akili? Jambo linalohusu ubinafsishaji.
=>Tangu rais huyu aingie madarakani anasema viwanda tutavirejesha serikalini na wananchi wnapenda kauli hii.
=> Na watu wakimshangilia naye anavimba kichwa.
=>Ni sera ya mtu asiyejua uchumi
=>Hakuna mfanyabiashara duniani ambaye atapewa kitega uchumi kinachoingiza faida akakifunga kwa sababu anaichukia Tanzania.
=>Hivi viwanda vilibinafsishwa baada ya serikali kushindwa kujienda. Vilikosa ruzuku ya Serikali Leo kuna Mkutano wa CHADEMA na Wanahabari unaofanyika Upanga kwenye Hotel ya Courtyard, Protea.
Huu ni Mkutano wa Uongozi wa Juu wa Chama na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari waandamizi, utakafanyika kuanzia Saa 04:30 asubuhi, katika hoteli ya Protea Courtyard
Hii inatokana na uamuzi ambao Kamati Kuu ya CHADEMA imeufanya katika mkutano wake wa siku mbili; tarehe 29-30 Julai, 2017 katika Hotel ya Double Tree, jijini Dar es Salaam.
Maeneo ambayo yamejadiliwa na kuridhia kuchukuliwa kwa hatua ni;
1. Hali ya mwenendo wa siasa katika nchi na ukandamizaji wa demokrasia unaofanywa na serikali ya awamu ya tano.
2. Kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha kwa Watanzania
3. Kamata kamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA maeneo mbalimbali nchi nzima.
Nimefika maeneo haya, ntahakikisha nawahabarisha kila kinachojiri. Karibuni.
No comments:
Post a Comment