Kesi ya kubenea yapigwa kalenda tena leo - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 26 July 2017

Kesi ya kubenea yapigwa kalenda tena leo

Kesi ya shambulio la kawaida inayomkabili Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (CHADEMA) imeahirishwa tena leo baada ya upande wa mashtaka kudai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Kubenea alifikishwa kwa mara ya kwanza Julai 5 katika mahakama ya wilaya ya Dodoma kwa kosa la kumshambulia mbunge mwenzie wa CCM, Juliana Shonza katika viwanja vya Bunge.

Hata hivyo wakili wa serikali, Foibe Magiri amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujamailika ambapo hakimu katika kesi hiyo James Karayemaha ameiahirisha hadi Agosti 23, mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena.

Katika kesi hiyo Kubenea aliwakilishwa na wakili Izack Mwaipopo kati ya mawakili watano wanaomtetea, mawakili wengine wanaomtetea Kubenea katika kesi hiyo ni Jeremia Mtobesya, James Ole Millya, Fred Kalonga na Dickson Matata

No comments:

Post a Comment

Popular