Ccm yaibomoa chadema team jimbo Hai mkoani Kilimanjaro - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 26 July 2017

Ccm yaibomoa chadema team jimbo Hai mkoani Kilimanjaro

Ndugu Humphrey Polepole akiwa mkoani Kilimanjaro amesema,kuna viongozi kadhaa kutoka upinzani hasa chadema wameikubali kazi na kasi ya Mhe. Rais Magufuri,lazima tuwapokee kwa heshima kubwa.
"Watu hawa wametumia Uhuru na haki yao ya kidemokrasia na kuamuua kuondoka katika vyama vyao na kujiunga na ccm,ni watu wazito sana" amesema Humphrey Polepole.
Humphrey Polepole aliwapokea na kuwataja viongozi hao waliotoka chadema na kuamia ccm ni madiwni watatu ambao ni
      (1) Diwani wa kata ya machame magharibi,mhe.Goodluck Kimaro ambaye ni makamu mwenyekiti wa wa wilaya ya ha(chadema),hivyo nimeamua kumuunga mkono Rais Magufuri
      (2)Diwani kata ya weruweru.
      (3)Diwani wa kata ya mnadani wilaya Hai.
Mhe.Evarist Peter Kimali amesema kuwa japokuwa walipata ushindi mkubwa 2015 lakini ndani ya chama kulitokea mpasuko uliosababishwa na uhujuma ndani ya uchaguzi wa ndani ya chama.
Katibu wa itikadi na uenezi wa ccm,ndugu Humphrey Polepole amesisitiza kuwa kuna lundo la viongozi wa upinzani wanaotaka kujiunga na ccm.

No comments:

Post a Comment

Popular