Cuf ya Maalim seif yajipanga kujibu mapigo ya Prof Lipumba - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 26 July 2017

Cuf ya Maalim seif yajipanga kujibu mapigo ya Prof Lipumba

Cuf upande wa Maalim Seif Sharif Hamad  amesema utaitisha baraza kuu la uongozi la Taifa kujibu mapigo ya profesa Lipumba.
Naibu karibu wa cuf -Zanzibar,Nassor Ahmed Mazrui alisema wamepata taarifa za baraza kuu hilo kwani kwamba wataitisha lakwao kujibu mapigo.
Mazrui alisema kabla ya kuitisha baraza kuu la uongozi la Taifa,kikao cha kamati ya utendaji itakutana kwaajili ya kujadili swala hilo kwa kina,na kuwataka wanachama wa cuf kuendelea kuwa wavumilivu.
"Tutaitisha baraza kuu la uongozi la Taifa halali kujadili hata yaliyofanywa na upande wa profesa Lipumba,hapo ninavyoongea na wewe ninaongoza kikao cha maandalizi kuhusiana na kamati ya utendaji na baraza kuu".
Baraza kuu la uongozi la Taifa  halali litatoa uamuzi wa nini mwelekeo na uamuzi uliofanywa na hawa watu ambao wengine tuliwasimamisha uanachama", alisema Mazrui ambaye ni mmoja kati ya viongozi watakaoitwa kwaajili ya mahojiano kwa tuhuma za kukihujum chama hicho kwa mujibu wa profesa Lipumba.

2 comments:

  1. Huyu tumbili keshamaliza miti sasa anakuja mwilini tafadhali ile sera ya jino kwa jino iwe activated na lolote liwalo naliwe aondoke msaliti buguruni kwa namna yoyote ili liwe funzo kwa wote wale wanaotumiwa na siasa za divide and rule

    ReplyDelete
  2. Huyu tumbili keshamaliza miti sasa anakuja mwilini tafadhali ile sera ya jino kwa jino iwe activated na lolote liwalo naliwe aondoke msaliti buguruni kwa namna yoyote ili liwe funzo kwa wote wale wanaotumiwa na siasa za divide and rule

    ReplyDelete

Popular