Wataalamu wa jiolojia wamesema kuwa tetemeko la ardhi limetokea kata ya Aneti wilayani Chamwino mkoani Dodoma usiku wa kuamkia jana lina ukubwa wa 5 katika kipimo cha richter.
Tetemeko lenye ukibwa wa 5.1 kipimo cha richter lilitokea julai mwaka juzi katika kata hiyo na kusababisha nyumba zaidi ya 60 kupata nyufa.
Ofisa mwandamizi wa jiolojia katika wakala wa jiolojia nchini (GST), Gabriel Mbogoni alisema tetemeko hilo limetokea katika maeneo lilipotokea mwaka jana, tetemeko hilo lilitokea kusini mashariki mwa kata ya Aneti.
Alipoulizwa kama tetemeko hilo lilitokea saa 9 usiku limeleta madhara yoyote, Mbogoni alisema hajapata taarifa ya kutokea madhara yoyote.
"Ukubwa wa 5 siyo la kawaida. Unakumbuka la Bukoba lilikuwa na ukubwa gani? Ni kama 5.7 kwa kipimo cha richter, tetemeko linaweza likawa na ukubwa wa tano hadi saba lakini lisilete madhara yoyote",alisema Mbogoni.
Mbogoni alisema tetemeko hilo linaweza likawa na ukubwa mdogo lakini likaleta madhara kutegemea na mpasuko wa miamba imetokea katika kina gani?.
" Inategemea pia na eneo ambalo mawimbi yanapita, ile miamba iko namna gani",alisema Mbogoni.
Alifafanua kuwa tetemeko hilo liliga kati ya sekunde nne mpaka sekunde tano kwamba likipiga kati ya sekunde 20 hadi 30 madhara yake yangekuwa makubwa sana.
Mbogoni alisema madhara hayo yanatokana na jengo kutikiswa kwa muda mrefu ambao tetemeko linadumu.
Mkuu wa wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga alisema hadi jana mchana kulikuwa hakujaripotiwa madhara yoyote.
"Nimewasiliana na viongozi wa kule, diwani na mwenyekiti wa kitongoji wanaseama ni kweli lilitokea lakini hadi sasa hakujaripotiwa madhara yoyote", alisema mkuu wa wilaya Vumilia.
Tetemeko kubwa la ardhi kutokea nchini lilitokea miaka tisa iliyopita lilitokea katika eneo la Oldonyo Lengai ambalo lilikuwa na ukubwa wa 5.9 kwa kipimo cha richter

No comments:
Post a Comment