Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia Mohammad bin Salman anaripotiwa kutumia wakala kununua moja kati ya michoro ghali zaidi duniani katika mnada uliofanyika mjini New York katika hali ambayo anawabana wananchi na kuwakamata matajiri na wanawafalme kwa madai ya ubadhirifu.
Duru za kijasusi nchini Marekani zimeliambia gazeti la Wall Street Journal siku ya Alhamisi kuwa, Mohammad bin Salman ndiye mnunuzi wa siri wa mchoro maarufu wa zama za Renaissance uliochorwa na Leonardo da Vinci na ambao ni maarufu kama Salvator Mundi. Bin Salman ameununua mchoro huo wa Kikristo kwa dola milioni 450 hii ikiwa ni rekodi mpya duniani.
Mgeni akichukua picha ya Salvator Mundi' wa Leonardo da Vinci katika Jengo la Mnada la Christie New York , Novemba 15, 2017.
Mchoro huo, unaoaminika kuchorwa miaka 500 iliyopita, ni wa Yesu (Nabii Issa AS) na Mrithi wa Ufalme wa Saudia ameununua kupitia wakala wake, mwanamfalme Bader bin Abdullah bin Mohammed bin Farhan Al Saud. Duru zinasema mchoro huo utahifadhiwa katika jengo jipya la makumbusho la Louvre, mjini Abu Dhabi.
Mchoro huo umenunuliwa katika hali ambayo bin Salman amewakamata wanawafalame na wafanyabiashara zaidi ya 200 kwa tuhuma za kuhusika na ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma. Aidha utawala wa Saudi Arabia unatekeleza sera za kubana matumizi ambazo zimepelekea bei za huduma za kimsingi nchini humo kupanda kwa kasi huku raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini humo wakilazimika kutozwa kiasi kikubwa cha fedha ili kupata kibali cha kuishi katika ufalme huo.

No comments:
Post a Comment