Vitendo kama vile kuzuia kurushwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya bunge, kufungiwa kwa baadhi ya vyombo vya habari, kufikishwa mahakamani kwa Watanzania sita kwa madai ya kumtukana Rais na kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa, vinasababisha wananchi kuona hakuna demokrasia nchini.
Baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 Rais Magufuli alipiga marufuku mikutano ya siasa na kusema kuwa wakati wa siasa umeisha na sasa ni wakati wa kazi na kuwataka wanasiasa ambao wameshinda kwenye majimbo yao husika ndiyo kufanya mikutano ya kisiasa.
June 2 2016 Jeshi la polisi nchini lilitoa tamko lililolenga kuzuia mikutano, maandamano ya kisiasa nchini kutokana hali za kiusalama kutokuwa sawa.
Katiba inaruhusu raia kukusanyika mahali popote mradi tu wasifunje sheria( Right assembly). Ndio maana tunakusanyika misibani, makanisani, misikitini,mahakamani,viwanjani,n.k.
Hapa nchini Tanzania Katika Ibara ya 20(1) ambayo inasema “kila mtu ana haki ya kukusanyika kwa uhuru na amani, kujihusisha na kushirikiana na watu wengine, kwa minajili hiyo kutoa maoni hadharani na kuunda na kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kulinda au kudumisha imani au maslahi yake mengine”
Kwa ujumla zipo sheria na kanuni zinazoelekeza ni namna gani watu wanaweza kukusanyika na hata kufanya maandamano ya amani ili kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa kwa walengwa. Mara nyingi tumeshuhudia polisi ambao kazi yao kubwa ni kulinda usalama wa raia na mali zao, wakitumia nafasi yao isivyostahili kwa kuwanyanyasa raia badala ya kuwalinda, kama kaulimbiu yao inavyobainisha.
Ni vyema kwa Serikali kulinda haki hii ya kikatiba ya kukusanyika, kwa kuimarisha ulinzi kwa wananchi wanapohitaji kukusanyika kwa ajili ya shughuli za kijamii hata shughuli za kisiasa na kiuchumi.
Jeshi la polisi kufuata sheria na kutumia busara katika kusitisha maandamano ya wananchi badala ya kutumia nguvu kupita kiasi. Jeshi la polisi linapaswa kuwa na mfumo thabiti wa kuimarisha ulinzi na Usalama pale wananchi wanapotaka kutekeleza haki yao ya kuandamana kama ilivyopambanuliwa katika Katiba.

No comments:
Post a Comment