Serikali kutoa Mafunzo Maalum kwa watafuta Ajira Wasio na Uzoefu. - KULUNZI FIKRA

Friday 18 May 2018

Serikali kutoa Mafunzo Maalum kwa watafuta Ajira Wasio na Uzoefu.

 
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa Leo  Mei 18,2018, Bungeni Jijini  Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Mhe Anthony Mavunde amesema serikali kwa kushirikiana waajiri na wafanyakazi watawapeleka vijana kujifunza katika makampuni mbalimbali kwenda kujifunza miezi 6 hadi mwaka mmoja na baada ya kumaliza watatoa cheti kama reference ya kigezo cha Experince

Mhe Mavunde amesema “Ni kweli kumekuwepo na changamoto kubwa uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi ambazo zinaombwa kama itakumbukwa wakati wa kampeni mwaka 2015 Mhe  Rais pia aliwahi kulisemea hili juu ya kigezo cha uzoefu, sisi kama Wizara tukaona kwasababu asilimia kubwa ya vijana wanaotoka katika vyuo vikuu na elimu ya juu wamekuwa wakipata tabu sana kwenda kujifunza kwa vitendo,” amesema Mhe Mavunde.

“Kama serikali tukaona sehemu ya kwanza ni kuhakikisha tunatengeneza  muongozo huu na muongozo huu tumefanya kati ya serikali, waajiri na vyama vya wafanya ili kutoa nafasi wale wahitimu wa vyuo vikuu wakimaliza masomo yao  na tumeshazungumza na makampuni yanatoa nafasi tunawapeleka moja kwa moja katika makampuni na Taasisi mbalimbali kwenda kujifunza kuanzia miezi 6 hadi mwaka mmoja na kumpatia cheti cha kumtambua  lengo letu ni kuondokana kikwazo cha kigezo cha experience ili akitoka pale akienda sehemu awe na  reference.”amesema Mhe Mavunde.

Kwa upande wake, Waziiri Sera, Bunge, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Mhe Jenista Muhagama alisema kuwa, Baada ya serikali kuona tatizo hilo wameshatengeneza hiyo miongozo lakini wanafikiri sasa kazi yao kubwa ambayo wameanza kuifanya ndani ya ofisi ya Waziri Mkuu nikujilink kama ofisi ya Waziri Mkuu na miongozo waliyonayo ili kuhakikisha tunawaandaa hawa vijana kuingiza katika soko la ajira.

“Tumekubaliana pia ndani ya serikali pia ndio maana mmeona matangazo ya ajira yanayotolewa sasa hivi kimsingi wanaoajiriwa ni wale fresh kabisa kutoka vyuo vikuu na Taasisi nyingine ambazo zinatengeneza ujuzi , lakini wakati mwingine tunaweza tukawa tunataka ajira katika position fulani ambazo zina matakwa rasmi kwa mfano Mkrugenzi fulani kwa matakwa fulani,” ameongeza Jenista.

Aidha alisema serikali baada ya kuona nafasi hiyo wameanza kulifanyia kazi eneo hilo na tunawaondoa ofu vijana kuwa kwasasawanataka kuwapa assuarence bila kupata vikwazo vyovyote katika nchi.

No comments:

Post a Comment

Popular