Naibu waziri wa Afya, Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa si kila mtu ana mamlaka ya kuiagiza Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA).
Dkt Ndugulile ameyasema hayo leo Mei 2, 2018, alipokuwa akizindua Bodi tendaji ya kwanza ya maabara ya mkemia mkuu wa Serikali.
Dkt Ndugulile ameitaka bodi hiyo kusimamia na kuhakikisha elimu inatolewa kwa wananchi ili waelewe namna sahihi ya utendaji wake.
Pia Dkt Ndugulile amesema miaka ya hivi karibuni vinasaba vimekuwa vinaongelewa zaidi lakini jamii haitambui, taratibu na namna wanavyoweza kufuata taratibu na kupimwa.
Dkt Ndugulile amesisitiza kuwa elimu ianze kutolewa kwa jamii kuelewa mwenye mamlaka ya kuviomba hivyo vipimo na kuielekeza maabara ya mkemia mkuu kuvipima.
"Tusije kufungua mambo ambayo hayapo, si kila mtu ana mamlaka ya kuiamrisha maabara ya mkemia mkuu kupima na kutoa majibu, kuna taratibu zake," amesema Dkt Ndugulile.
Dkt Ndugulile ameeleza kuwa elimu itasaidia kila mtu kujua nani anapaswa kufanya nini wakati gani na kwa sababu gani.
"Haya mambo ni ya kisheria, ukikosea kuchukua vipimo, kuagiza vipimo kesi hata kama ipo mahakamani inafutwa" amesema Dkt Ndugulile.
"Siyo kila mtu anaweza kuiamrisha maabara ya mkemia mkuu kufanya vipimo vya vinasaba,’’ amesema Dkt Ndugulile.

No comments:
Post a Comment