Waziri Mkuchika atoa wito kwa wanaume wanaowazalisha wake zao Ovyo. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 18 April 2018

Waziri Mkuchika atoa wito kwa wanaume wanaowazalisha wake zao Ovyo.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe  George Mkuchika amewataka wanaume kuacha kuwazalisha wake zao mara kwa mara ili kulinda afya za wanawake hao.

Mhe Mkuchika amesema suala la kuzaa mara kwa mara linamfanya mwanamke kukosa muda wa kupumzika na kushindwa kumlea kwa nafasi mtoto anayezaliwa.

Waziri amesema Serikali inatoa likizo ya uzazi kwa wanawake waliojifungua ya siku 84 na muda huo ni kwa wanawake waliojifungua katika kipindi cha miaka mitatu tangu alipojifungua mtoto mwingine.

Katika swali la msingi,Mhe Sonia Magogo mbunge wa Viti Maalumu alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia kinamama ambao wanajifungua kabla ya kipindi cha kuruhusiwa kuzaa tena  ambacho ni miaka mitatu.

Waziri amesema mtumishi akijifungua watoto mapacha ataongezewa siku 14 na kufikia likizo ya siku 98.

"Endapo mtumishi atajifungua mtoto/watoto kabla ya kutimiza miaka mitatu ya matenite, atapewa likizo  maalumu ya wiki sita ili kuhudumia mtoto wake kwa mujibu wa kanuni za kuhudumia utumishi wa umma za mwaka 2009," amesema Mhe  Mkuchika.

Kuhusu watumishi wa sekta binafsi, amewataka kuangalia sheria za nchi ili kuwapa nafasi wafanyakazi wa sekta binafsi likizo ambayo ni haki yao ya msingi

No comments:

Post a Comment

Popular