Polepole afunguka mengi kuhusu wanaopotosha Ripoti ya CAG. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 18 April 2018

Polepole afunguka mengi kuhusu wanaopotosha Ripoti ya CAG.

 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole amesema kuwa kuna viongozi wa upinzani wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kuupotosha umma, tabia ambayo haikubaliki, haivumiliki na itafika wakati watasema sheria ichukue mkondo wake maana wanaleta taharuki kwa wananchi.

Hamphrey Polepole amesema hayo Leo Jumatano Aprili 18, 2018,  wakati akifafanua mambo kadhaa yanayopotoshwa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).

Polepole amesema imekuwa tabia na mtaji wa kiongozi huyo ambaye hakumtaja jina kutoa taarifa za uongo.

“Kiongozi unasema fedha zimeibiwa sijiu akiambiwa atoe ushahidi atasemaje. Siku hizi hana hoja ana kazi ya kuleta taharuki kwa umma,” amesema   Polepole.

“Hatuko tayari kuendelea kuona watu wachache wauhadaa umma.”amesema Polepole.

Pia Polepole amesema CCM hakiamini malumbano, mabishano yasiyo na tija, lugha za kubeza, kebehi na kufifisha moyo wa kizalendo kwa Watanzania.

“Nchi yetu ina mfumo wa kidemokrasia ya vyama vingi lakini CCM inaendelea kuamini sisi ni wamoja.” amesema Ndugu Polepole"Sasa unaposoma taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) halafu unatoa kauli timilifu kuwa pesa imeibiwa, yaani pesa ya Umma imeibiwa", amesema Polepole.

"Tunaweza tukakwambia tusaidie kuthibitisha sasa ukishindwa umesema uongo umeuhadaa Umma, umetoa takwimu za uongo ukichukuliwa hatua sio ndiyo utaanza kusema uongozi huu hatuna huruma, huruma kwa watu waovu? Waongo wanaopotosha kwa makusudi hilo halikubaliki", amesema  Polepole.

 Polepole a akaendelea kusema, "Mimi sielewi huyu anayekwenda mbele kusema taarifa za uongo uongo hivi, ndiyo mtaji wake siku hizi anatafuta tu pahala. hoja hana, hazungumzi kuhusu rushwa siku hizi".

"Hazungumzi kuhusu huduma za kijami, hazungumzi kuhusu ufisadi, hazungumzi kuhusu miundombinu, tunapiga hatua kubwa, tunapeleka watoto shule bure, bali yeye anatafuta hoja ya uongo uongo" alisema Polepole

Polepole katika mkutano huu ameeendelea kumtuhumu mtu huyo kushindwa kuwa na uhakiki wa maneno yake.

"Kuna kipindi mtu huyu alizungumza kuhusu njaa, wewe unaijua njaa inatangazwa vipi sasa tumevumilia sana leo tumeshindwa tumeona tumsaidie kumuelewesha halafu tuseme wale ambao wana dhamana ya kuhakiki maneno tunayatoa kwa kweli wachukue hatua kwani hatupo tayari kuacha watu wachache waendelee kuudanganya umma wa watanzania hili halikubaliki" alisisitiza  Polepole.


Polepole amesema anaipongeza serikali ya CCM kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuweka hadharani ripoti ya CAG na kuchukua hatua kwa wanaofanya ubadhirifu unaobainishwa

Polepole anaipongeza serikali kwa kuwa Rias Magufuli alipochukua hatua za awali, mawaziri nao walifuta hatua hizo na kuwachukulia hatua maafisa kwenye wizara zao

Polepole amesema pia vipo vyama vya siasa vinatumia fedha ya umma na havitoi hesabu na kusemainabidi vichukuliwe hatua kali za kinidhamu

Amesema vipo vyama vimetumia zaidi ya Sh. milioni 700 bila kutoa hesabu, pia vipo vyma ambavyo vinatumia fedha bila kufuata kanuni za kihasibu

Kuna chama kinaitwa ABC, SAU, Chadema wametumia fedha bila kutoa hesabu zilivyotumika na pia kutumia fedha zaidi ya bilioni 2.2 bila kupeleka benki na kuhoji vinawezaje kuikosoa serikali?

Pia Chadema imefanya manunuzi ya zaidi ya bilioni 24 bila kushindanisha wakati ndio hao wanaoisema serikali

Polepole anasema isiidhie kuwataja kwenye taarifa ila msajili achukue hatua, hata kama ni ndani ya CCM

Polepole amesema inapotoshwa kuwa CCM imekopa ndani ya mifuko ya hifadhi ya jamii, CCM ina utaratibu wake wa ndani wa kulinda maslahi ya watumishi wake tofauti na vyama vingine

CCM ina utaratibu wa kulimbikiza fedha kila mwisho wa mwezi ili watumishi wake wanapomaliza utumishi, ipo fedha ya kuwalipa mafao yao

Katika akaunti ya CCM inayosimamiwa na Baraza la wadhamini walitoa zaidi ya milioni 300 ili watumishi wanaaondoka walipwe na wanazirudisha ili mfuko uendelee kunona

Amesema Chadema wamepotosha juu ya hili na wanapaswa kuchukuliwa hatua

Polepole pia anasema serikali ya CCM sasa ina utaratibu wa kuweka hesabu za serikali katika mtindo jumuishi, zamani zilikuwa zikitolewa kwa wizara na taasisi moja moja lakini kwa sasa unaweza kuzipata katika sehemu moja

Tanzania ni nchi ya pekee kufanya hivyo katika Afrika Mashariki na hii inasaidia kuweka mambo wazi zaidi na mtindo huu ni mgumu

Polepole amesema Zitto Kabwe ndio anaongoza kupotosha ripoti ya CAG kwa kukurupuka naripoti asizozielewa, na kusema Taarifa ya CAG ilikuwa imeshapitiwa na wao kwanza

Polepole anasema anapotosha kuwa trilioni 1.5 zimepotea na kufafanua kuwa sasa kuna mtindo mpya ambao unafuata vigezo vya kimataifa vya ukaguzi wa hesabu za umma unaitaka serikali inapokagua fedha zake zinapoingia kuhesabu pia na pesa baada ya serikali kuwa imetoa huduma ,

zamani ilikuwa ni lzaima ipokee fedha kwanza ndipo ihesabu fedha imeingia, ila sasa huduma inapotolewa hata kama fedha haijakusanywa inahesabiwa (acrrual basis)

Makusanyo ghafi ni makusanyo ya jumla, baada ya makusanyo ghafi inatakiwa ukokotoe ujue makusanyo sahihi ni yapi

Tumekusanya trilioni 25.3, pesa ambayo huduma imetolewa na inatarajiwa imekushwa kuingizwa kwenye jumla hiyo

ukitaka kujua makusanyo halisi unachukua trilioni 25.3 unatoa makusanyo tarajiwa (receivables)

Unachukua trilioni 25.3 unatoa bilioni 687.3 (receivables) kama hatua kupata makusanyo halisi
Pia unatoa bilioni 203.92 ambazo ni fedha zilizokusanywa kwa ajili ya Zanzibar, ambayo haisomwi kwenye bajeti ya Serikali ya Muungano

Ukitoa hesabu hizo unapata Shilingi trilioni 24.4 hizi ndio makusanyo halisi ya mwaka 2017/208

Zitto anadai pesa zilizotumiaka kutoka trilioni 25.3 ni trilioni 23.79, hii kipindi mkaguzi anapita zilikuwepo fedha za serikali ambazo zilikuwa kwenye hatifungani (zilikuwa hazijaiva) ambayo ni shilingi 697.85 bilioni

Ukichukua 697.85 bilioni ukijumlisha trilioni 23.5 unapata trilioni 24.4, na ukichukua 25.3 ukatoa 23.79 unapata 1.5 trilioni ambayo ndio zitto anadai imeibiwa

Polepole anasema Zitto hajui hesabu na anapaswa kumtafuta mwalimu

Polepole anasema pia Zitto amepotosha kuhusu bilioni 219 ambayo ililipa madeni ya zamni ambayo hayakuwa yamepitishwa na Bunge

Amesema haesabu za serikali zinawekwa kwenye vifungu, na kulikuwa na madeni ya watu mbalimbali yanayofikia bilioni 969 ambayo yalipitishwa na Bunge na serikali inayalipa baada ya kuyahakiki, bilioni 219 ni sehemu ya bilioni hizo 969 zinazofahamika na Bunge pia

Polepole amesema Zitto amepotosha pia kuhusu serikali kukopa bilioni 500 ambazo ni zaidi ya ukomo iliyowekewa, amsema hili hatajibu analiachia Bunge, hayo mawili ameyazungumzia ili kumpa elimu

Polepole amesema Zitto achukuliwe hatua kwa kupotosha na ni kwa sababu alikuwa amezoeshwa vibaya

Mwisho wa wiki iliyopita, Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Mhe Zitto Kabwe aliizungumzia kwa mapana zaidi taarifa ya CAG na kuonyesha mambo ambayo serikali imetuhumiwa kufanya ikiwa pamoja na upotevu wa fedha zaidi ya Trilioni 1.5 ambayo haina maelezo imetumikajePolepole amesema anaipongeza serikali ya CCM kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuweka hadharani ripoti ya CAG na kuchukua hatua kwa wanaofanya ubadhirifu unaobainishwa.




No comments:

Post a Comment

Popular