Wasanii wafanyakufuru baada ya mazishi ya Marehemu Agnes Masogange. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 24 April 2018

Wasanii wafanyakufuru baada ya mazishi ya Marehemu Agnes Masogange.

Baadhi ya wasanii walioshiriki maziko ya msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ jana Aprili 23, 2018 walijivinjari maeneo kadhaa ya starehe jijini Mbeya.

Johari, Aunt Ezekiel, MC Pilipili, Belle 9, Dogo Janja ni miongoni mwa wasanii waliotembelea kiwanja cha Mwailubi Car Wash & Lounge, kilichopo Forest ya Zamani.

Belle 9 saa sita usiku aliondoka na kwenda New City Pub, eneo la Mwanjelwa.

Wasanii hao waliondoka wakiwa kwa makundi baadhi wakiendelea kujivinjari hadi usiku wa manane.

Mwanamuziki Belle 9 mchana wa Aprili 23, 2018 wakati wa mazishi alishindwa kuimba wimbo wa Masogange ambao ndiyo ulimtambulisha Agnes na kumpa jina la Masogange.

Tofauti na mchana wakati wa mazishi ambapo wasanii hao walikuwa tayari kupiga picha na mashabiki, usiku waliwagomea.

Uwepo wa wasanii hao ulikuwa neema kwa baadhi ya wamiliki wa maeneo ya kuuza vileo ambao walieleza kuwa mauzo yameongezeka.

Pasipo kutaka kutaja jina, mmiliki wa pub moja alisema, “Hii ni heshima kwetu, maana si kitu rahisi kundi kubwa la wasanii hawa maarufu nchini kuja kunywa na kufurahi hapa.”

Masogange alifariki dunia Aprili 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam na alizikwa jana Aprili 23, 2018 nyumbani kwa baba yake, Utengule- Mbalizi wilayani Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Popular