Rais Magufuli ataja Changamoto Nne EAC. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 24 April 2018

Rais Magufuli ataja Changamoto Nne EAC.

 
Rais John Magufuli amezitaja changamoto nne zinazoikabili Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwamo vikwazo vya kiuchumi uwekezaji, ukosefu wa viwanda, kutoaminiana ndani ya jumuiya hiyo na ujenzi wa miundombinu.

Rais Magufuli ameyasema hayo Leo Aprili 24, 2018, alipokuwa akihutubia Bunge la Afrika Mashariki (Eala) katika mkutano wake wa nne kikao cha kwanza ulioanza jana mjini Dodoma ikiwa ni mara ya kwanza vikao vya bunge hilo kufanyika mkoani humo. Pia ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuhutubia bunge hilo.

Pia Rais Magufuli amesema mbali na mafanikio, jumuiya hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo migogoro ambaye amesema imegharimu maisha ya watu wengi.

Aidha, Rais Magufuli ametaja changamoto nyingine kuwa ni vikwazo vya kibiashara na uwekezaji kuwa bado vipo na kutokuaminiana ndani ya wanachama wa jumuiya hiyo.

“Mara nyingi huwa hatupendi kuyasema sema haya lakini mimi nayasema ili muyabebe na mjue hiyo chalenji, pamoja na changamoto nyingine nyingi mnapaswa muanze kuzitoa mapema,” alisema  Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Popular