ACT-wazalendo wamwandikia Barua IGP Sirro. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 24 April 2018

ACT-wazalendo wamwandikia Barua IGP Sirro.

Chama cha ACT-wazalendo Wazalendo kimesema kimepokea taarifa katika mitandao ya kijamii kuhusu tishio la kuuawa kwa Kiongozi wake, Mhe Zitto Kabwe.

Katibu wa Itikadi, Mawasiliano kwa Umma na Uenezi, Ado Shaibu amesema taarifa hizo hawakuzipuuza na tayari chama kimemuongezea ulinzi Zitto, ili kukabiliana na tishio hilo.

Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 23, 2018 wakati wa mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam.

"Lakini tumemwandikia barua IGP ili achunguze taarifa hizo, hatuwezi kupuuza kwa sababu Chadema ililalamika kabla ya shambulio la Tundu Lissu, hatupuuzi kwa sababu, leo hii hatujui Ben Saanane yuko wapi," amesema Shaibu.

Katika hatua nyingine, Shaibu amesema ACT-wazalendo imebaini udanganyifu wa Serikali katika ufafanuzi wa sakata la Sh1.5 trilioni.

Pia Shaibu amesema baada ya kuchunguza, ACT-wazalendo kimebaini akaunti ya Zanzibar pamoja na Hesabu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa mwaka unaoishia Juni 30 mwaka jana, hazionyeshi taarifa ya Sh203 bilioni kupelekwa Zanzibar.

Ufafanuzi bungeni wiki iliyopita, naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Ashantu Kijaji alitaja maeneo matatu ya kutumika kwa Sh1.5 trilioni, akisema kati ya fedha hizo Sh203 bilioni zilikuwa ni makusanyo ya kodi kwa ajili ya Serikali ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Popular