Wakati wadau wa elimu wakijadili kauli za marais wastaafu kuhusu hali mbaya ya elimu, Serikali imesema iko tayari kwa mjadala huo ili kuboresha.
Juzi, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza katika kongamano lililopewa jina la Mageuzi ya Afrika katika Karne ya 21 lililofanyika Harvad nchini Marekani, alisema Afrika inaweza kuwa inapiga hatua katika elimu lakini inahitaji kuongeza juhudi hasa kutoka elimu ya msingi hadi sekondari akisema ni asilimia 20 tu ya vijana wanaoweza kwenda sekondari na kibaya zaidi hata hao wachache, hawafanyi vizuri.
Kauli hiyo imekuja mwezi mmoja tangu Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kutaka kuwapo kwa mjadala wa kitaifa kuhusu elimu kutokana na matokeo mabaya kwa shule za Serikali.
Jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk Leonard Akwilapo alisema Serikali inakaribisha mjadala huo.
“Mjadala haukatazwi kwa sababu unatatua matatizo. Kwani watu wakikaa na kujadili turekebishe hapa na pale kuna ubaya gani?” alihoji Dkt Akwilapo.
Akiunga mkono hoja ya mjadala, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) ambaye pia ni waziri kivuli wa elimu, Suzan Lyimo alisema wameshazungumza kuporomoka kwa elimu muda mrefu na Serikali inaonekana kuziba masikio.
“Ukifuatilia hotuba zangu kama waziri kivuli bungeni nimesema kwamba elimu yetu iko ICU (chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi) lakini hatusikilizwi. Lakini kwa kuwa wamesema Kikwete na Mkapa labda ndiyo watasikiliza. Je, Serikali itakubali huo mjadala wanaoutaka?” alisema Lyimo, “Kila waziri anayekuja kwenye elimu analeta mikakati yake.”
Alisema kutokana na mfumo huo kuwa mbovu, wanafunzi wengi wanaomaliza shule za sekondari hawajui hata kusoma na kuandika sawasawa wala kujieleza.
Mbunge wa Vunjo ambaye pia ni mdau wa elimu, James Mbatia alisema alishaeleza bungeni mwaka 2013 juu ya janga lililopo kwenye elimu lakini hoja yake haikufanyiwa kazi na Serikali.
Januari 31, mwaka huu katika kikao cha Bunge, Mbatia aliwasilisha hoja binafsi kuhusu udhaifu katika sekta ya elimu akielezea kwa kina, sera ya elimu iliyopitwa na wakati, kukosekana kwa mitalaa, kuwapo kwa mihtasari mibovu ya masomo na vitabu kuwa na viwango duni.
Mbali ya kuwasilisha hoja hiyo, mwaka huohuo, NCCR Mageuzi, chama anachokiongoza, kilimwandikia barua Rais Kikwete wakati huo, kikimuomba aunde tume ya kudumu ya elimu nchini.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Tenmet, Cathleen Sekwao aliunga mkono hoja ya kuwapo kwa mjadala akirejea matatizo ya mara kwa mara waliyoishauri Serikali bila mafanikio.
“Zamani mwalimu alikuwa na uwezo wa kumfikia kila mwanafunzi, lakini siku hizi wanafunzi ni wengi, mwalimu anaishia kuandika ubaoni na kuondoka,” alisema Sekwao.
Alisema kwa sasa, walimu wanatakiwa watumie mtalaa unaompa uwezo mwanafunzi kutumia masomo kujikimu kimaisha, lakini hata walimu wenyewe hawaujui.

No comments:
Post a Comment