Tasnia ya sanaa imezizima. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya msanii aliyekuwa akipamba video za muziki (video vixen au video queen), Agnes Gerald ‘Masogange’ kufariki dunia juzi.
Pamoja na maisha yake ya mitandao ya kijamii, kutuma picha na kuandikwa magazetini kwa matukio mbalimbali, lakini kuna mambo kadhaa usiyoyajua kumhusu mrembo huyo.
Masogange alifariki juzi majira ya saa tisa katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Msanii huyo anatarajia kuagwa leo katika Viwanja vya Leaders Club, kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba na kisha kusafirishwa kwenda Utengule mkoani Mbeya na atazikwa Jumatatu kijijini hapo.
Kwa ufupi, haya ni baadhi ya usiyoyajua kuhusu Masogange.
Mtoto wa mwanajeshi
Mwananchi jana lilifika nyumbani kwa Masogange ulipo msiba wake na ilifanya mahojiano na kaka yake aitwaye David Mpori ‘Bonny’.
Bonny alibainisha kuwa Masogange alizaliwa 1988 kwa baba yake anayeitwa Gerald Waya aliyekuwa dereva wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na alistaafu mwaka 1980.
Kwa sasa mzee Gerald ameamua kujikita kwenye kilimo katika Kijiji cha Utengule, Wilaya ya Mbalizi mkoani Mbeya.
Nyota huyo alilelewa na mzazi mmoja tangu akiwa na miaka miwili.
Bonny alisema Masogange alilelewa na baba tangu akiwa na miaka miwili, baada ya wazazi wake kutengana mwaka 1990.
Hata hivyo, alipohitimu masomo yake ya kidato cha nne alikuja jijini Dar es Salaam na kuishi kwa shangazi yake mpaka pale alipoanza kujitegemea.
Asili ya jina Masogange
Jina la Masogange ni la kupachikwa. Alilipata jina hilo kutokana na wimbo wa mwanamuziki Belle 9 wa mwaka 2011 ambao ulipewa jina Masogange
Belle 9 aliliambia gazeti hili jana kuwa msiba huo umemshtua.
Alisema, “Masogange’ ni neno la Kiganda linalomaanisha macho yangu. Ni mimi ndiye nilitoa jina la wimbo kwa sababu wakati huo muziki wa Uganda ulikuwa juu zaidi,” alisema.
Baada ya kuonekana katika wimbo huo, ndipo jina la Agness lilipoanza kufifia na Masogange likapata umaarufu. “Ni miongoni mwa watu ambao walinifanya nipae kimuziki kwa sababu ule (wimbo) wa Masogange ulikuwa ni wimbo wangu wa pili kuutoa,” alisema.
Mwanamuziki huyo alisema anashukuru kwa sababu jina la wimbo wake ndilo limekuwa mtu maarufu.
Aliishi na nyota watatu
Wakati kukiwa bado na siri nzito ni wapi hasa wanandoa Irene Uwoya na Dogo Janja wanaishi, ukweli ni kwamba walikuwa wakiishi jengo moja la ghorofa na Agnes, lililopo maeneo ya Makongo Juu.
Mbali na Uwoya, pia inaelezwa ndipo yalipokuwa makazi ya nyota wa bongo fleva, Aslay Isihaka ambaye hata hivyo amehama hivi karibuni.
Ana mtoto wa darasa la saba
Wakati wasanii wengine kila wakati wakiwaweka watoto wao katika mitandao ya kijamii, kwa Masogange ilikuwa tofauti. Wachache ndiyo waliofahamu kuwa alikuwa na mtoto anayesoma darasa la saba. Mwandishi wetu alimuona mtoto huyo jana msibani akiwa katika majonzi makubwa.
Mzaliwa wa Mbeya
Kwa mujibu wa Bonny, Agnes alizaliwa mkoani Mbeya na alisoma Shule ya Msingi Utengule na baadaye kujiunga na Sekondari ya Meta.
“Alipomaliza kidato cha nne alifunga safari na kuja jijini Dar es Salaam kwa shangazi yake aliyeishi Magomeni na hapo ndipo alipoanza kutafuta fedha hadi kushiriki kwenye video za muziki kama ‘video queen’,” alisema akiongeza kuwa na baadaye pia alijichanganya kwenye filamu.
Alipanga kuzindua nyumba
Kwa mujibu wa ndugu mwingine wa Masogange, Flora Mwamlima, Masogange alikuwa tayari amemjengea nyumba baba yake eneo la Utengule na alitarajia kuizindua Desemba.
“Alitarajia kwenda kuifanyia uzinduzi Desemba mwaka huu, lakini ndiyo hivyo Mungu kaamua kumchukua mapema zaidi, lakini shughuli za mazishi zitafanyika hapo,” alisema.
Baada ya kesi alibadilika
Flora alieleza kuwa Masogange alibadilika baada ya kesi yake ya kutumia dawa za kulevya kwisha.
“Baada ya kuponea chupuchupu kwenda lupango kutokana na kukabiliwa na kesi ya dawa za kulevya, Masogange aliamua kubadili mfumo wake wa maisha na makazi yake yakawa ni kanisani na nyumbani,” alisema. Flora alisema katika kipindi hicho kifupi pia aliacha kwenda katika kumbi za starehe kama ilivyokuwa kawaida yake.
Mambo mengine
Mwaka 2013, Masogange alikamatwa na dawa za kulevya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini akiwa na mwenzake, Melissa Edward.
Mwaka 2017, alikamatwa na baadaye mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimkuta na hatia ya kutumia dawa za kulevya.

No comments:
Post a Comment