Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wanawake waliotelekezewa watoto kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi cha mvua ili mradi kila mtoto apatiwe haki yake inayostahili kama alivyoahidi japokuwa anajua kuna wanaume wanaomba dua mvua iendelee kunyesha ili mambo yaharibike
Paul Makonda ametoa kauli hiyo leo Aprili 13, 2018 alipokuwa akizungumza na umati mkubwa wa mama ambao mpaka sasa hawajafanikiwa kupata namba ya kuingia ndani kusikilizwa shida zao na kuwasii wamama hao kuwa na subira wapatiwe namba ili zoezi hilo liweze kuendelea kusudi kila mmoja apate haki yake.
"Furaha niliyonayo nikuona kuna watu wameshaanza kupata amani ya mioyo yao na hilo ndio lilikuwa lengo kubwa la serikali yenu na watumishi hawa waliojitolea ambako kiukweli siwalipi hata senti 5", amesema Makonda.
"Lakini zaidi ya yote ndio lengo la Mungu kuleta amani katika familia. Leo ni siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ya mwisho lakini ukitazama kuna watu hata namba hawajapata lakini kuna mambo mawili lazima muyapate", amesema Makonda.
Pamoja na hayo, Makonda ameendelea kwa kusema "jambo la kwanza ni lazima kila mtoto apate kile anachostahili, jingine ni kupata bima ya afya niliyoahidi kwa kila mtoto aliyekanyaga katika viwanja hivi. Kwasababu hizo niwaombe muwe wavumilivu leo wote ambao hamjapewa namba mtapewa.
"Vumilie mvua najua wakina baba huko walipo wanaombea mvua iendelee kunyesha ili mambo yaharibike lakin waambieni kama mliweze kuvumilia miezi tisa na matusi yote waliyowatukana sembuse mvua ? kwa hiyo tutaendelea kuvumilia mpaka haki itakapopatikana", amesema Makonda.
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema mpaka kufikia siku ya tano leo wameshasikilizwa takribani wamama 4,000 huku familia 205 kwa hesabu za siku ya jana (Alhamisi) yaani watoto 205 wameondokana na mfumo wa omba omba na sasa wanapatiwa huduma zote zinazostahili kwa baba na mama zao wakiwa pamoja.
Pia wanawake 178 waliofika kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kulalamikia kutelekezwa na baba za watoto wao, wamepatanishwa na wazazi wenzao.
Hayo yalibainishwa Mkuu huyo wa Mkoa, alipokuwa anazungumzia mafanikio yaliyopatikana tangu kuanza kwa kampeni hiyo, Jumatatu iliyopita.
Makonda alisema, hatua hiyo ni nzuri kwa kuwa lengo kubwa la mkakati wake ni kusaidia upatikanaji wa haki ya kwanza ya watoto, ambayo ni malezi ikifuatiwa na haki nyingine kama vile upendo na ukaribu.
“Kwa hiyo katika hilo la upendo na ukaribu kwa sasa naweza kusema kuwa limerejea kwa kuwa kama wazazi wote wawili wamekutanishwa na kukubaliana kuendelea na mahusiano yao, hakika mtoto atakuwa mwenye furaha,” amesema Makonda.
atakuwa mwenye furaha,” alisema Makonda.
Aidha Makonda amesema tangu kazi hiyo ianze hadi sasa, ofisi yake imewahudumia wanawake zaidi ya 1,498 na ana imani lengo la kuwahudumia wanawake wote waliojitokeza litatimia.
Pia Makonda aliweka wazi kuwa hadi sasa, wapo wanaume ambao wamekubali kupimwa vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa watoto wanaoambiwa kuwa ni wao. Wakati huo huo, Makonda amezungumzia ujio wa kongamano kubwa la wafanyabiashara wa Ufaransa Jumatatu ijayo.
Vile vile Makonda amesema, kampuni 30 za wafanyabiashara kutoka Ufaransa, zitashiriki kwenye kongamano hilo litakalofanyika jijini Dar es Salaam, ambalo kwa kiwango kikubwa litaongeza chachu katika mpango wa serikali wa kufikia uchumi wa kati.

No comments:
Post a Comment