Baba amnywesha mwanae wa miezi miwili sumu ili kulinda ndoa. - KULUNZI FIKRA

Friday, 13 April 2018

Baba amnywesha mwanae wa miezi miwili sumu ili kulinda ndoa.

Mtoto wa miezi miwili  amenusurika kifo baada ya kunyweshwa sumu ya panya na baba yake mzazi,  Edson Damian (37) aliyetaka kuficha siri kwa mkewe wa ndoa kwani mtoto huyo amemzaa nje ya ndoa yake.

Mama wa mtoto huyo anaeleza kuwa alipobaini kuwa mtoto kapewa sumu alikimbia kwa jirani anayefuga ng’ombe, ndipo akachukua maziwa akamnywesha, na baadae alichukua bodaboda hadi Kituo cha Polisi kupewa RB na kisha kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kupatiwa matibabu, na sasa mtoto wake ni mzima anaendelea vizuri.

Mwanaume huyo ni Katibu wa CCM, Kata ya Kitangili inadaiwa kuwa wakati anamtongoza Mzazi mwenzake huyo alimhakikishia kuwa hana mke na baada ya kuzaa mtoto huyo ndipo alianza kumkataa na kusema ameoa na hamtaki kwani atamvunjia ndoa yake.

Mtuhumiwa huyo anashikliwa na Jeshi la Polisi, upelelezi ukikamilika atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazomkabili.

No comments:

Post a Comment

Popular