Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amevitaka vyombo vya dola kufanya kazi kwa kuheshimiana katika kesi inayomkabili Harbinder Seth na James Rugemalira, akihoji sababu za Seth kutopelekwa katika matibabu kama ilivyoagizwa.
Seth na Rugemalira wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Dola za kimarekani 22, 198,544.60 (Sh309.5bilioni) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Akizungumza leo Jumatano Aprili 11, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, hakimu Shaidi amesema haipendezi kila mara amri za mahakama kutoheshimiwa, kusisitiza kuwa chombo hicho cha dola kinafanya kazi kwa mujibu wa sheria.
Amesema hata Seth ambaye ni mshtakiwa wa kwanza akitazamwa tu anaonekana wazi kuwa ni mgonjwa, kutaka suala la ugonjwa wake aachiwe daktari.
Hakimu Shaidi ametoa kauli hiyo baada ya wakili wa Serikali, Nassoro Katuga kueleza kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na kwamba bado hawajatekeleza agizo lililotolewa na mahakama la kumpeleka Seth Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu.
Katuga amedai Seth aliomba wakati anapelekwa MNH, daktari wake wa Afrika kusini awepo.
Amesema kwa sasa wanasubiri taarifa kutoka kwa mshtakiwa kuhusu daktari wake na kwamba sababu nyingine iliyowafanya washindwe kutekeleza agizo la mahakama kwa wakati ni mshtakiwa kuhamishwa kutoka gereza la Segerea kwenda gereza la Ukonga.
Wakili wa utetezi, Hajra Mungula amedai kuwa mshtakiwa hajaongea chochote na kwamba wanashtushwa na maneno yaliyotolewa na upande wa mashtaka.
Mungula amedai kuwa agizo la mahakama wakati linatolewa Machi 28, 2018 tayari mshtakiwa huyo alikuwa amekwishapelekwa gereza la Ukonga.
Amesema hali ya Seth si nzuri na kwamba suala la afya si la mzaha, “hatuwezi kuendelea na kesi mtu akiwa mgonjwa.”
Amedai mshtakiwa ana daktari wake wa familia na kwamba daktari huyo alishtushwa baada ya kuona picha ya mshtakiwa Seth, ameomba wakati Seth akisubiri kupelekwa hospitali amfanyie vipimo na dawa ambazo anatakiwa kupatiwa.
Wakili huyo amedai kuwa imekuwa ngumu kwenda kumuona gerezani na hata kumpa dawa, kwamba hawajui upande wa mashtaka unadhamira gani.
Aliomba kukabidhi dawa za Seth upande wa mashtaka lakini haruhusiwi mtu yeyote kumuona hata mke wake wa ndoa na kuomba mahakama iliangalie hilo.
Baada ya Wakili Mungula kueleza hayo, Wakili wa Rugemalira, Cuthbeth Tenga amedai amri za mahakama zinachukuliwa kirahisi na kila siku upelelezi haujakamilika na akaomba aambiwe upande wa mashtaka wana nia gani na washtakiwa.
Amedai kuwa kamishna wa magereza aitwe mahakamani aje aeleze kwanini amri za mahakama hazitekelezwi.
Akijibu hoja hizo, Wakili Katuga amedai si nia ya upande wa mashtaka kuwaweka watu ndani bila kuendelea na shauri na kwamba wana nia ya dhati lakini mazingira yake yanachelewesha upelelezi.
Katuga amedai kuwa agizo limetolewa na mahakama wanalifanyia kazi na wakati mwingine hakutakuwa na malalamiko na wataeleza hali ya upelelezi ilipofikia.
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 25, 2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

No comments:
Post a Comment