Lema amekamatwa na Jeshi la polisi. - KULUNZI FIKRA

Friday, 27 April 2018

Lema amekamatwa na Jeshi la polisi.

Mbunge wa Arusha Mjini Mhe  Godbless Lema leo April 27, 2018 amekamatwa na  Jeshi polisi na kufunguliwa kesi mpya kuhusu uchochezi kwa ndoto aliyowahi kuota kuhusu Rais Dkt John Pombe Magufuli miaka miwili iliyopita.

Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amethibitisha hilo na kusema kuwa Lema leo alihudhuria Mahakamani kwa ajili ya kesi iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka miwili iliyopita.

"Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limemkamata Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwa kile kinachodaiwa "uchochezi". Dhidi ya Mhe  Rais kuhusiana na ndoto aliyowahi kuota.

Mhe Lema alihudhuria Mahakamani siku ya leo kwa ajili ya kesi iliyokua ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka 2 iliyopita. Baada ya Mahakama kufuta kesi hiyo leo na kuachiwa...Polisi walimkamata tena na kumfungulia kesi upya kwa mashtaka yale yale" alisema John Mrema

Kesi hii ni mwendelezo wa kesi iliyokua ikimkabili Mhe  Godbless Lema na ambayo ilimsotesha Mahabusu (Magereza) kwa zaidi ya miezi 4 mwaka juzi kabla ya kuachiwa kwa dhamana mapema mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

Popular