Watu wawili wafariki dunia katika ajali ya Basi la polisi kugongana na gari dogo. - KULUNZI FIKRA

Friday, 27 April 2018

Watu wawili wafariki dunia katika ajali ya Basi la polisi kugongana na gari dogo.

Mwanajeshi mmoja wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  pamoja na mtoto wa Mwanajeshi mwenzake wanadaiwa kupoteza maisha katika ajali iliyohusisha gari la Polisi aina ya Basi lililogongana na gari dogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), maeneo ya Bwawani Morogoro

Inadaiwa basi hilo la Polisi lilikuwa likitokea Dodoma huku Noah hiyo iliyokuwa imebeba Wanajeshi takribani 6 pamoja na mtoto wa Wanajeshi mwezao ilikuwa ikitokea Morogoro.

Akiongea na mwandishi wa habari wa kulunzifikra blog Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ingawa amekiri kutokuwa na taarifa za undani zaidi kwa sasa hivyo endelea kufuatilia tutakujuza zaidi juu ya tukio hili.

No comments:

Post a Comment

Popular