Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva amesema tume hiyo ni huru isipokuwa ni maono ya watu kwa kutokuwapo neno ‘huru’.
Jaji Lubuva amesema hata nchi ambazo tume zao zina neno huru, kwa uhalisia si huru kwa sababu uchaguzi wao umekuwa ni wa vurugu.
Jaji Lubuva ambaye alipata kuwa Mwanasheria wa Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na baadaye Tanzania Bara, alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Oysterbay, Dar es Salaam juzi.
“Nisingependa sana kulizungumzia hili kwa sasa kwa sababu wenzangu wapo wangelizungumzia", alisema Jaji Lubuva.
“Lakini hata hivyo ni kweli mwenyekiti na makamishna wote wa tume wanateuliwa na rais, lakini tangu iliponzishwa mwaka 1992 tume ilikuwa ikifanya kazi zake kwa uhuru", alisema Jaji Lubuva.
“Haikuwahi kuingiliwa na mtu yeyote, ni huru na inasimamia uchaguzi kwa uhuru bila kuelekezwa na mtu yeyote aliyeko madarakani, hiyo ndiyo maana ya tume huru",alisema Jaji Lubuva.
“Iko hoja usipoandika tume huru kama ya Kenya, unaweza kuona kwamba pamoja na kutajwa kwenye sheria ni huru kumbe haziko huru hata kidogo", alisema Jaji Lubuva.
“Kilichopo ni maono ya watu, kwenye fikra zao wanafikiria kwamba mwenyekiti, wakurugenzi na makamishna wa tume wote wanateuliwa na rais hivyo wanadhani kwamba watapendelea mtu fulani", alisema Jaji Lubuva.
“Lakini kwa ukweli tume yetu ni huru pengine kuliko za nchi nyingine …na Kenya mlishuhudia ilivyokuwa ingawa tume yao ina neno huru,”alisema Jaji Lubuva.
Mwanasheria huyo nguli alisema kama ni kubadilishwa ni suala la kuangalia muda muafaka kwa sababu inahusu katiba.
“Sasa kama ni kubadilishwa ni suala la kuangalia muda muafaka kwa sababu ni suala la katiba, lakini jinsi katiba na sheria zilivyo nasema kwa nguvu zote kuwa tume yetu ni huru", alisema Jaji Lubuva.
“Tumekaa miaka minne na JK (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete), lakini hajawahi kuniita hata siku moja akanipa maelekezo yoyote kuwa pendelea fulani. Bila hata neno huru tume iko huru kabisa,”alisisitiza Jaji Lubuva.
Aprili 12, 2018, mwaka huu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai alitupilia mbali hoja ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), kuhusiana na marekebisho ya masuala yanayohusu Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Akizungumza bungeni baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu, alisema anaikataa taarifa ya mbunge huyo na akajipange upya.
“Kwa hiyo taarifa yako Mhe Kubenea naikataa kwa hiyo kajipange tena, kama bado una nia, uje katika utaratibu unaotakiwa kama hatukukuelewa tutatafuta muda tueleweshane zaidi ila sisi tumeelewa hivyo", alisema Spika Ndugai.
“Mheshimiwa Saed Kubenea ameleta kusudio la kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka Bunge lifanye marekebisho ya masuala yanayohusiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)", alisema Spika Ndugai.
“Ili ikidhi matakwa ya mfumo wa vyama vingi nchini sasa kwa kuwa Tume hiyo ya Taifa ya Uchaguzi imeanzishwa na Katiba katika ibara ya 74 marekebisho yote juu ya tume hiyo yanatakiwa kuletwa kwa kupitia muswada wa marekebisho ya Katiba na siyo hoja binafsi ya mbunge,” alisema Spika Ndugai.
Spika Ndugai alisema alichokisema Kubenea ni jambo linalohusu Katiba hivyo upo utaratibu wa kuafuata kuendana na mabadiliko hayo ya katiba ya nchi.
Spika Ndugai, alisema wabunge wamekuwa wakipata shida ya jinsi ya kuwasilisha hoja binafsi.

No comments:
Post a Comment